The House of Favourite Newspapers

Umafia! Kaze, Ntibazonkiza Wamvuta Yanga Mrundi wa Simba

0

WAKATI wakiwa kwenye pilika za kumshusha beki wa kati wa Chipa United ya Afrika Kusini, Frederic Nsabiyumva, Simba wamekutana na kigingi, kwani nyota huyo ameeleza kuvutiwa zaidi na Yanga.

 

Imeelezwa kuwa sababu ya beki huyo kuvutiwa na Yanga ni uwepo wa Warundi wenzake klabuni hapo ambao ni kocha mkuu, Cedric Kaze na fowadi, Said Ntibazonkiza. Nsabiyumva amekataa kujiunga na Simba inayomuwania katika usajili wa dirisha dogo.

 

Simba ilielezwa kuwania saini ya beki huyo mwenye umbo kubwa aliyepo kwenye kikosi cha Timu ya Taifa ya Burundi kilichoifunga Taifa Stars zilipocheza mchezo wa kirafi ki kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam, hivi karibuni.

 

 

Simba ipo kwenye mipango ya kusajili beki mmoja wa kati mwenye uzoefu wa michuano ya kimataifa ambayo watashiriki. Na chaguo lao la kwanza lilikuwa ni Nsabiyumva ambaye hata hivyo imeelezwa ameikataa ofa yao.

 

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Jumatatu, beki huyo malengo yake ni kuendelea kucheza soka la kimataifa zaidi ikiwemo Ulaya na siyo Afrika tena.

 

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa Simba hivi karibuni ilipeleka ofa ya kumhitaji beki huyo ambaye yeye aliwaambia kama akitaka kuja kucheza soka nchini Tanzania, basi bora akajiunga na Yanga na siyo kwenda huko. Aliitaja sababu ya beki huyo kuichezea Yanga, ni uwepo wa Warundi wenzake Kaze na Ntibazonkiza, maarufu kama Saidoo.

 

“Simba isahau kwa Frederic, kwani hii ni mara ya pili kuonyesha nia ya kutaka kumsajili, kutokana na ndoto zake alizonazo za kucheza soka la kulipwa zaidi ya Afrika Kusini alipo. “Kwani malengo yake ni kucheza soka la kulipwa Ulaya, hivyo kuja kucheza Tanzania anaona kama anajirudisha nyuma kimaendeleo, kama atahitaji kuja kucheza soka nchini, basi ni bora akajiunga na Yanga yenye ndugu zake wengi Warundi.

 

“Yanga ina kocha Kaze na Ntibazokinza wote raia wa Burundi ambao ndiyo wanamshawishi kuja kuichezea lakini siyo kucheza Simba ambayo imepeleka ofa nzuri,” alisema mtoa taarifa huyo. Alipotafutwa Katibu Mkuu wa Simba, Dk Arnold Kashembe kuzungumzia hilo, simu yake ya mkononi iliita bila kupokelewa.

 

Lakini Simba kwa kupitia Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Mohammed Dewji, hivi karibuni ilisema wamepanga kufanya usajili wa wachezaji zaidi ya watatu. “Kwa kuanzia, tumepanga kusajili kiungo mmoja mkabaji atakayekuja kuchukua nafasi ya Fraga (Gerson),” alisema Dewji hivi karibuni katika mkutano wake na wanahabari.

WILBERT MOLANDI NA IBRAHIM MUSSA, Dar es Salaam

Leave A Reply