Umewahi Kusikia au Kuona Bomba la Kupitisha Pombe? Soma Hapa

Waandalizi wa Tamasha maarufu la muziki wa rock nchini Ujerumani wamewahakikishia wateja zaidi ya elfu 75 kwamba, katu! hawatokumbwa na kiu ya pombe. Ujenzi wa bomba hilo kubwa ni maalum kwa ajili ya kusafirisha pombe katika eneo la tamasha hilo.

Waandalizi wa tamsha hilo maarufu kwa jina, Wacken Open Air festival, wanasema bomba hilo litakuwa na uwezo wa kufikisha glasi sita za pombe kwa kila sekunde ambapo bomba hilo litakuwa na urefu wa kilomita 7 na upana wa inchi 14.

Watu elfu 75 huwa wanahudhuria tamasha hilo kila mwaka, na inakadiriwa kwamba kila mmoja huwa anabugia lita tano za pombe katika kipindi cha siku tatu.

Toa comment