The House of Favourite Newspapers

VIDEO: Ummy Mwalimu Asema Dawa Zipo za Kutosha

waziri-afya-4-001Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akisoma taarifa.waziri-afya-3Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Rugambwa, akifafanua jambo.

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, amekanusha taarifa  kwamba kuna uhaba wa dawa za binadamu  nchini akisema kuwa taarifa hizo si za kweli bali zinalenga kuupotosha umma kwani zipo nyingi na zinaendelea kuingia.

 

Hayo yameelezwa na waziri huyo leo alipokuwa akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam juu ya taarifa zilizoripotiwa  kwamba serikali ina uhaba wa dawa.

Amesema hakuna upungufu wa dawa muhimu za binadamu kwani kuna dawa za kutosha na vifaa tiba na akaeleza bajeti yake ilikuwa chini ya shilingi bilioni 29 mwaka 2015/16 hadi kufikia bilioni 251 ikiwa ni zaidi ya mara tano.

Amefafanua kuwa chanjo za watoto ndizo zilikuwa zimeisha lakini napo walitoa taarifa kuufahamisha umma, na hivi sasa tayari zimekwishaletwa.

Kwa taarifa kamili tembelea Global TV Online kujua alichokisema waziri huyo.

Comments are closed.