The House of Favourite Newspapers

Ummy Mwalimu: Katika Watanzania 100, Watano Wana Maambukizi ya VVU

world-aids-day

UKIMWI bado ni janga kubwa nchini kwetu. Takwimu zinaonyesha maambukizi ya VVU kwa upande wa Tanzania Bara kuwa ni #asilimia5.3. #WanawakeNdioWameathirikaZaidiNaVVU (wastani wa asilimia 6.2% kulinganisha na asilimia 3.8 ya wanaume walioathirika).

Ufafanuzi zaidi kuhusu takwimu hizi ni kuwa:-

#Katika kila watanzania 100, watanzania 5 wana maambukizi ya VVU.

#Katika kila wanawake 100 Tanzania, wanawake 6 wana VVU

#Katika kila wanaume 100 nchini, wanaume 4 wana VVU.

Hali ni mbaya zaidi kwa vijana wenye 15 – 24. Maambukizi kwa kundi hili ni asilimia 10.6 Yaani ktk #KilaVijana100WenyeMiaka15-24, #Vijana11wanaMaambukiziYaVVU.

mwalimu

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu.

#Huduma za Dawa
Wanaopata dawa za kupunguza makali ya UKIMWI ni asilimia 50.

#Mwelekeo wa Kupambana na UKIMWI
Katika kufikia malengo ya kutokomeza UKIMWI duniani ifikapo 2030, Shirika la Umoja wa Mataifa linaloratibu mapambano dhidi ya UKIMWI (UNAIDS), limeweka malengo ya muda wa kati ya tisini tatu (90-90-90).

90 – asilimia 90 ya watu wote wanaokisiwa kuwa na VVU wajue hali zao.

90 – asilimia 90 ya waliobainika kuwa na VVU kuanza kutumia dawa mara moja.

90 – asilimia 90 ya walioanza dawa waweze kuwa na ufubazo endelevu wa virusi vya UKIMWI mwilini mwao.

#Rai yetu kwa Watanzania
– Serikali inawahimiza wananchi kuendelea kujitokeza kupima afya zao ili wajitambue na kujua namna ya kujilinda.

– Pia tunahimiza wananchi kuchukua hatua za kujikinga na maambukizi ya VVU. Jitihada kubwa zinefanyika za kuwaelimisha wananchi kuhusu VVU/UKIMWI. Kila mmoja wetu achukue hatua kwa kuepuka vitendo hatarishi vinavyoweza kusababisha kupata maambukizi.

TOPSHOTS Indian sandartist Sudersan Pattnaik gives the final touches to a sand sculpture on the eve of World AIDS Day, as a horseman rides by on Golden Sea Beach in Puri, some 65 kms east of Bhubaneswar on November 29, 2013. World AIDS Day is celebrated on December 1, every year to raise awareness about HIV/AIDS and to demonstrate international solidarity in the face of the pandemic. AFP PHOTO/ASIT KUMARSTRDEL/AFP/Getty Images ORG XMIT:

#DawaKwaKilaMwenyeVVU
Kwa upande wetu, Wizara ya Afya wajibu ulio mbele vyetu ni kuhakikisha wale wote ambao wanakutwa na maambukizi ya VVU, wanapata huduma ya dawa za kufubaza virusi vya UKIMWI mara moja ili waweze kuishi Maisha marefu na yaliyo na afya bora.

Maelekezo ya Shirika la Afya Duniani (WHO) yanazitaka nchi zetu kuwaanzishia dawa mara moja watu wote watakaopima na kugundulika wana VVU, yaani “Test and Treat”. Wizara ya Afya imeshatoa waraka wa kuanza mpango huu tangu Oktoba 2016. Mpango huu unatarajiwa kuongeza mahitaji ya huduma za matibabu na dawa.

People walk near a red ribbon sand sculpture created by Indian sand artist Sudarshan Patnaik on the eve of World AIDS Day on a beach in the eastern Indian state of Odisha November 30, 2012. REUTERS/Stringer (INDIA - Tags: SOCIETY HEALTH TPX IMAGES OF THE DAY) ORG XMIT: DEL11

Kwa sababu badala ya kuwa wanaotakiwa kupata dawa za kupunguza makali ni wale wenye CD4 count chini ya 500, sasa itakuwa yoyote atakaepima na kukutwa na VVU anatatakiwa kuanzishiwa dawa mara moja. Hili si jambo dogo. Linahitaji Rasilimali za Kutosha hasa Rasilimali za ndani.

Hivyo, ninapongeza jitihada zilizofanywa na Ofisi ya Waziri Mkuu/TACAIDS za kuanzisha Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI (AIDS Trust Fund). Hatua hii ni muhimu sana kwa nchi yetu ktk kutimiza wajibu tulionao wa kutoa huduma za tiba kwa waathirika wa VVU.

#TuunganeWoteKuzuiaMaambukiziMapyaYaVVU

Ummy Mwalimu, Mb.
WAMJW
Dar es salaam
1 Dec. 2016

halotel-strip-1-1

Comments are closed.