The House of Favourite Newspapers

Umoja wa Ulaya Wafanya Maonesho ya Wanaotaka Kwenda Kusoma Ughaibuni

0

 

Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, Manfredo Fanti akizungumza na wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

 

Umoja wa Ulaya (EU) na wawakilishi wa nchi wanachama waliopo nchini Tanzania, leo wamefanya Maonesho ya Elimu ya Umoja wa Ulaya 2022, yaliyofanyika katika Ukumbi wa Nkurumah uliopo katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

 

Maonesho hayo yanatoa fursa za masomo ya juu kwa vijana wa Kitanzania kwenda kusoma katika nchi za Umoja wa Ulaya ambapo pamoja na mambo mengine, wanafunzi waliohudhuria wamefundishwa  kuhusu fursa zilizopo kwa wanafunzi wanaotaka kwenda kusoma ughaibuni.

 

Dr. Evaristo Andreas Mtitu, Afisa Mwandamizi wa Elimu ya Juu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teklonojia.

 

Wanafunzi hao wamekutanishwa na wawakilishi kutoka nchi na taasisi mbalimbali za Umioja wa Ulaya, wanafunzi watarajiwa na wahitimu ambao wamewaeleza kuhusu fursa za programu za digrii ya wahitimu, kozi fupi, ufadhili wa masomo, ushirika na fursa zingine za kujifunza na utafiti, zinazotolewa na taasisi za EU au kuungwa mkono na nchi wanachama.

 

Baadhi ya wanafunzi walioshiriki katika maonesho hayo.
Leave A Reply