Umoja wa Waandishi Wanawake wa Binti Shupavu Wagawa Taulo za Kike na Kutoa Somo

Kiongozi wa Kundi la Binti Shupavu Khadija Seif Mbembe akizungumza na wanahabari baada ya hafla hiyo.

 

 

UMOJA wa waandishi wa habari wanaounda kundi la Binti Shupavu wametoa wamezungumza na mabinti wa Shule ya Msingi Msasani A, juu ya masuala ya hedhi salama na kujitambua kisha kuwagawia wanafunzi hao taulo za kike pedi.

Bondi Selemani Kidunda akigawa taulo za kike kwa mabinti wa Shule ya Msingi Msasani.

 

 

Akizungumza na wanafunzi hao kiongozi wa kikundi hicho, Khadija Seif Mbembe amesema lengo la kikundi chao ni kuhakikisha kuwa mabinti wote wanajiamini na kuwa shupavu.

Katika hafla hiyo mgeni rasmi alikuwa Bondi maarufu hapa wa uzito wa kilo 75 Selemani Kidunda ambaye naye aliwapa somo wanafunzi hao. Akizungumza na mabinti hao alisema;

Kiongozi wa Binti Shupavu, Khadija Seif akitoa somo kwa mabinti hao.

 

 

“Lengo umoja wetu ni kuhakikisha mbinti wanasimama wenyewe na kuepuka vishawishi ambavyo vinaweza kuwaharibia maisha yenu.”

“Mnapopatwa na changamoto ikiwemo suala la hedhi haraka muwajulishe walimu wenu au walezi huko majumbani na msije mkawahusisha watu wengine huko mitaani mfano madereva wa bodaboda na wengineo”.

Mwalimu Mkuu wa Shule ua Msingi Msasani, Edward Mollel akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) kwenye hafla hiyo.

 

 

Jamii ya watu kama hao wanaweza kukusaidia shida yako lakini na wao ni lazima kuna kitu watahitaji kutoka kwako jambo ambalo linaweza kuwaingiza kwenye mtego wa ngono na kuishia kwenye maradhi ya ukimwi na mimba hivyo kuharibu ndoto za maisha yenu”.

Kati yenu hapa naamini kuna watu ndoto zao ni kuwa marais, madaktari, mainjinia na fani nyinginezo sasa ukipata mimba au ukimwi katika umri mlio nao hamtaweza kutimiza ndoto zenu nafikiri mmenielewa mabinti wazuri.” Alisema Khadija.

Afisa Ustawi wa Jamii Kata ya Msasani Manispaa ya Kinondoni, Kachiki Njovu akizungumza na mabinti hao na kuwapa elimu ya hedhi salama.

 

 

Nae Bondia Selemani Kidunda amewaambia mabinti hao kuwa wanapokuwa na changamoto hususan katika wanapokuwa katika hedhi wasihofie kuwaeleza hata wazazi wao wa kiume kwakuwa kwa ulimwengu wa sasa suala la hedhi siyo siri, aibu wala si ugonjwa hata baba pia nae ni mlezi hivyo inapotokea changamoto au mahitaji ya taulo za kike ni bora kumshirikisha kuliko kwenda kuwashirikisha madereva wa bodaboda huko mitaani ambao kama mlivyoelezwa na madam Khadija.

 

Pia Kidunda alitumia nafasi hiyo kuwahamasisha Watanzania kumpa sapoti kwenye pambano lake la marudiano na bondia Katompa kutoka nchini Congo DR linalotarajiwa kufanyika Julai 30 mwaka huu.

Akizungumza kwenye hafla hiyo mwalimu mkuu wa Shule ya Msingi Msasani Edward Mollel amesema ameupokea kwa furaha ugeni huo shuleni hapo.

 

“Nisema nimeupokea kwa furaha kubwa sana ugeni na zawadi hizi walizotuletea ambazo zitapunguza changamoto kwa mabinti ambao familia zao hazina uwezo wa kununua taulo hizo kila zinapohitajika na kuziomba taasisi zingine na watu binafsi kuiga mfano huu wa wanahabari hawa wa Binti Shupavu”. Alisema Mwalimu Mkuu Mollel.

4229
SWALI LA LEO
YANGA/SIMBA KIMATAIFA
Baada ya usajili wa nguvu, mechi za Siku ya Wananchi na Simba Day kisha mechi ya ufunguzi wa Ligi Kuu ya Ngao ya Hisani, je, ni timu gani unaamini itafanya vizuri kimataifa?Toa comment