The House of Favourite Newspapers

Umoja wa Walima Mboga Wazungumzia Kampeni ya ‘Kijana Inuka’

0
Mhamasishaji wa kilimo cha mbogamboga, Asifa Saidi (kulia) akizungumza Jambo.
Mwenyekiti wa Chama cha mbogamboga, Josephy Kunguru (kulia) akizungumza Jambo.
Wanahabari wakiwa katika kikao hicho.

NA DENIS MTIMA/GPL

UMOJA wa Kilimo cha Mbogamboga,  Matunda na Nafaka wa jijini Dar es Salaam, umezungumzia kampeni yao ya Kijana Inuka na kilimo chenye lengo la kuepukana na kilimo cha kutegemea.

Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa chama hicho, Josephy Kunguru, alisema kuwa kilimo hicho ni kilimo cha biashara  kinachohitaji maji na miundombinu ya uhakika.

Alisema kuwa watu wengine wamekuwa wakiogopa kuwa kilimo hicho ni ghali sana na kinahitaji watu wenye pesa nyingi, jambo ambalo si kweli kwani kitu cha msingi ni kuzingatia masharti  ya namna ya kuhifadhi kilimo hicho.

“Tunatakiwa tuungane katika kilimo hiki ili tuwafanye wananchi kulima kilimo chenye tija badala ya kulima kwa kutegemea mvua,”  alisema akiongeza kuwa umoja huo una zaidi ya wanachama 74 wote wakitokea wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam.

Leave A Reply