The House of Favourite Newspapers

UN: MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA YAONGEZEKA AFRIKA

OFISI ya Kupambana na Mihadarati ya Umoja wa Mataifa imesema katika ripoti yake mpya kwamba matumizi ya madawa ya kulevya yameongezeka mara 10 katika kipindi cha kuanzia mwaka 2014 hadi 2017 huko magharibi mwa Afrika.

Ofisi ya Kupambana na Mihadarati na Uhalifu ya Umoja wa Mataifa (UNODC) imetoa ovemba 3, 2019 ilitoa ripoti maalumu na huku ikitahadharisha kuhusu kuongezeka matumizi ya aina mbalimbali za madawa ya kulevya magharibi mwa Afrika imesema kuwa, kiwango cha mihadarati kilichokamatwa kuanzia mwaka 2014 hadi 2017 katika ukanda huo kimeongezeka mara 10.

Ripoti ya ofisi hiyo iliyoandaliwa na Jumuiya ya Kiuchumi ya Magharibi mwa Afrika (ECOWAS) kwa msaada wa kifedha wa Umoja wa Ulaya imeongeza kuwa, licha ya kuongezeka idadi ya opereseheni, kutiwa nguvu watu na kukamatwa aina nyingi za mihadarati, lakini matumizi ya madawa hayo haramu yameongezeka barani Afrika hususan magharibi mwa nchi hiyo. Ripoti hiyo imeongeza kuwa, kasi ya matumizi ya madawa ya kulevya katika nchi za Nigeria na Mauritania haioneshi dalili zozote za kupungua.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, asilimia 18 ya watu wanaopewa huduma za kuachana na madawa ya kulevya magharibi mwa Afrika wana umri wa baina ya miaka 10 hadi 19.

Ufukara wa kiuchumi na kiwango cha juu cha ukosefu wa ajira kwa upande mmoja, na kukosekana miundombinu mizuri ya masuala ya afya hasa katika nchi maskini za magharibi mwa Afrika kwa upande wa pili, ni indhari tosha ya kuzuka tsunami ya vifo vinavyotokana na matumizi ya mihadarati katika nchi hizo; karibuni tu hivi.

Comments are closed.