The House of Favourite Newspapers

UN: Riek Machar Ametimkia DRC

0

machar-newUmoja wa Mataifa umesema Makamu wa Rais wa zamani wa Sudan Kusini Riek Machar ambaye alikuwa haonekani hadharani yuko nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Taarifa zainasema Kikosi cha Majeshi ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa yaliyopo Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo yalimsaidia yeye, mke wake pamoja na wengine kutoka kwenye mpaka unaogawa nchi hizo mbili.

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir alimtimua kazi Bwana Machar mwezi uliopita baada ya mapigano baina ya majeshi yanayowaunga mkono na kusababisha maafa.

Taarifa zinasema Machar aliondoka Sudan Kusini kwa kuhofia usalama wake ikiwa ni siku chache baada ya kuzuka mapigano kati ya vikosi vyake na vile vinavyoitii serikali ya Juba.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa, Farah Haq, amesema Umoja wa Mataifa unatambua kuwa siku ya jumatano bwana Machar aliingia nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo kupitia mpaka baina ya Sudan Kusini na Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo na kusaidiwa na majeshi ya Umoja wa Mataifa ya kulinda amani ambayo baadae walimsafirisha kwa ndege hadi mji mkuu Kinshasa.

Afisa wa umoja wa mataifa amesema kwamaba bwana Machar alihitaji kusafirishwa kwa njia ya ndege kiusalama na hivyo amepatiwa huduma za kimatibabu

Awali msemaji wa Riek Machar alisema Hasimu huyu mkubwa wa Rais Salva Kiir aliingia nchini DR Congo lakini alikuwa na lengo la kuelekea Ethiopia.

Kwa mujibu wa shirika moja la habari la AP, umoja wa mataifa imeonyesha kuwa bwana Machar alikuwa Hatarini hivyo ukamaamua kumsaidia.

Awali Bwana Machar ataka majeshi yasioyoegemea upande wowote yatumwe nchini Sudan Kusini ili kuhakikishiwa usalama wake baada ya walinzi wake na walinzi wa Rais Salva Kiir kupigana.

Mamia ya raia wameuwawa na wengine zaidi ya laki moja wakikimbia nchi hiyo.

Leave A Reply