The House of Favourite Newspapers

#GlobalUpdates: Unaambiwa Watu Wengi Wenye Uwezo Asilia (Genius) Ni Wavivu Na Walevi – (Video)

Leo kwenye Global Updates za Machi 9 2017 inakuletea dalili au sifa kumi za watu wenye uwezo asilia maarufu kwa kiingereza kama ‘Genius people’. Zipo ambazo unazijua ila pia kuna hizi ambazo hujawahi kuzisikia na wala hutegemei.

Kwenye pitapita yangu YouTube nimekutana na video kutoka kwenye chanel ya Mind Warehouse walioipa jina ’10 Signs You’re Actually A Genius’, ndani ya video hiyo wameongelea sifa ama tabia 10 za watu wenye uwezo asilia.

Ukiachilia mbali sifa ya kuwa watu hawa huwa na uwezo mkubwa kiakili, ni watu wa kukesha na kusoma sana unaambiwa sifa zao nyingine kuu ni pamoja na hizi; uvivu, ulevi na uchafu.

Najua unachofikiria kuwa, ‘Mh! Hapana, haiwezekani!’, na ndio maana nikaona nikuweke video yake yenye dakika sita hapa chini ujiridhishe mwenywe.

Zijue Sifa Nyingine Za Watu Wenye Uwezo Asilia ( Genius People)

 

IMEANDIKWA NA: Sandra Brown

VIDEO/ YouTube: #Mind Warehouse

Subscribe kwenye YouTube Chanel yetu ya Global TV Online ili zote kali zinazotufikia iwe ni siasa, michezo, comedy, burudani, stori za mastaa, updates mbalimbalimuziki na nyingine zikufikie kwa wakati.

Comments are closed.