The House of Favourite Newspapers

Unajifanya kuzuga siyo? Soma hapa

0

blackcouple-bedsmileAsalaam aleikum wapendwa wasomaji wa safu yetu hii ya Shangingi Mstaafu. Najua mlikuwa mnanisubiri kwa hamu nije niwape mbili tatu za wiki iliyomalizika, lakini mnajifanya kama hamna habari na mimi.

Leo nataka nizungumze na mashosti zangu wale wanaojifanya wanaenda na wakati, mwezi mtukufu nao unawaona na ushungi kama wafungaji kweli, kumbe kazi yao ni kuvizia.

Ukimuona alivyovaa, anavyotembea, yaani haki ya Mungu unasema mtu si ndo huyu, lakini angalia balaa lake giza likiingia, anakuwa mtu mwingine kabisa. Yupo machimbo, anaendeleza mtungi kama kawaida, utasema mwezi hajauona.

Anakuwa kama kinyonga, asubuhi anapokwenda sokoni macho yanamchezacheza, hayatulii ilimradi wakware wanamjazia kikapu anavyotaka, muuza nyanya anatoa udenda, muuza nazi naye hoi, muuza mchele hali kadhalika, wanamjazia vitu vya futari kwa ahadi ya ‘ngoja mfungo uishe.’

Anarudi kapu limejaa, jioni naye anapika futari shosti na daku anaihubiri. Lakini cha kushangaza muda wa futari ukiisha tu, huyoo viwanja. Anatoka mtaani kavaa kama Ninja, akitoka machoni mwao, ‘shungi’ linawekwa kwenye mkoba, vimini vinachukua nafasi.

Nataka niseme na nyinyi mashosti zangu wa namna hii kwa sababu nina simulizi ya kutisha sana iliyompata mwenzetu mmoja hivi enzi zile za tukitingisha jiji kiwanja cha  Magoti.

Alikuwa anaishi Vingunguti, akahamia Magomeni, lakini viwanja kila siku tunakutana. Sasa kufika Migomigo, akawa mgeni, akienda sokoni anagombewa, sasa yeye akawa anajifanya kashika dini, hataki mambo ya uchafu eti hadi mwezi uishe.

Watu wakawa wanawekeza, kapu linajaa mivyakula, mtoto wa kike huyoo nyumbani. Usiku kama kawa, tunapigana vikumbo kuwagombea Wahindi na Wazungu. Sasa yupo bwana mmoja naye alikuwa miongoni mwa wale wawekezaji wa kule sokoni, kumbe naye yule bwana mtu wa mambo yetu, kaja!

Si kamkuta bi dada naye kajipanga mstari, akamtazama vizuri, akamgundua ndiye. Kwa vile alikuwa akimtaka siku nyingi, akamchukua. Mdada hakumgundua yule bwana, kaingia naye kwa Babu wakaachana!

Kesho yake bwana kapeleka simulizi kwa wenzake sokoni, kwamba kumbe si lolote, hakuna cha mshika dini wala nini ni kahaba wa kutupwa, akatoa ushuhuda wote alioujua.

Kesho yake hana hili wala lile, shosti kama kawaida yake, mbwembwe nyingi kaingia sokoni. Laiti angelijua, asingetoka nje siku hiyo, wakamzunguka, wakaanza kumzomea kahaba huyoo, huyooo kahaba, huyooo, rudisha vitu vyetu. Wakamtoa ushungi, wakamvua viatu, wakamzomea yaani aibu tupu.

Tangu siku ili akahama mtaa kwa aibu aliyoipata.

Leave A Reply