The House of Favourite Newspapers

Unajua kwa nini mimba inatunga nje ya kizazi?

0

wherefibroidsgrowBaada ya kupeana elimu juu ya tatizo la mawe kwenye figo, leo ningependa tupeane ufahamu kuhusu mimba kutungwa nje ya mji wa mimba. Wanawake wengi wamekuwa wakilalamika wanasumbuliwa na tatizo hili na imefika hatua wengine wanaogopa kujihusisha na uzazi kwa sababu ya tatizo hili.

Mimba kutunga nje ya mfuko wa uzazi wa mwanamke au Ectopic pregnancy ni tatizo ambalo limetokea kuathiri wanawake mbalimbali. Kuna watu wanaposikia na kusoma habari za mimba kutunga nje ya mji wa mimba wanachukulia ni kitu kisichowezekana na ni jambo la kutishiana.

Nikuhakikishie msomaji wangu kuwa hili ni miongoni mwa matatizo yanayowasumbua sana akina mama. Kwa kawaida, isipokuwa mara chache sana, mimba zitungazo nje ya mfuko wa uzazi hazina uwezo wa kukua kuwa mtoto kamili.

Aidha, mimba hizi ni hatari kwa afya ya mama mjamzito kwa vile humfanya kupoteza damu nyingi na hatimaye kusababisha kifo.

Katika mfumo wa uzazi wa mwanamke kuna sehemu nyingi ambazo kila moja ina umuhimu wake ikiwa sehemu mojawapo itapata hitilafu husababisha athari katika mfumo wa uzazi. Miongoni mwa sehemu muhimu sana ni Ovari ambayo ndiyo sehemu mayai ya uzazi yanapotengenezwa.

Mayai haya husafiri kupitia mirija ya Fallopian. Kazi za mirija ya Fallopian ni kusafirisha mayai kutoka katika kiwanda chake cha uzalishaji (ovary) mpaka kwenye mfuko wa uzazi (uterus). Utungisho wa yai la kike (ovum) na mbegu ya kiume (sperm) hufanyika kwenye mirija hii.

Usikose kufuatilia mada hii Alhamisi ijayo kwenye gazeti hilihili.

Leave A Reply