Unajua kwa nini mimba inatunga nje ya kizazi?-2

PainDuringpregnancyWiki iliyopita nilielezea sababu zinazofanya mimba itunge nje ya mfuko wa uzazi na kuzitaja. Leo naendelea na mada hii ili wasomaji wangu wapate kujifunza zaidi…

Mara baada ya utungisho, misuli inayozunguka mirija ya Fallopian ikishirikiana na vinyweleo vilivyopo ndani ya mirija hii husukuma kiinitete au yai lililorutubishwa na kulipeleka kwenye Uterus.

Yai lililorutubishwa au kiinitete, lifikapo kwenye Uterus hujipachika katika mojawapo ya kuta zake kwa ajili ya kuendelea kurutubishwa, kukua taratibu na hatimaye kufanya mtoto.

Inapotokea misuli hii kushindwa kufanya kazi au vinyweleo hivi kukosekana, kiinitete hushindwa kusafirishwa kuingia kwenye Uterus na hivyo hujitunga nje ya Uterus na kusababisha Ectopic Pregnancy. Karibu asilimia 1-2% ya mayai yaliyorutubishwa hutunga nje ya mfuko wa uzazi wa mwanamke.

λ Aidha, zaidi ya asilimia 95% ya mimba zinazotunga nje ya Uterus hutokea kwenye mrija wa Fallopian. Mimba zinazotunga kwenye mrija huo husababisha kiinitete Embryo kujipachika katika kuta zake na hivyo kusababisha mishipa ya damu inayopita karibu na mrija wa Fallopian kupasuka na damu kutoka kwa wingi hali ambayo isiposhughulikiwa mapema husababisha madhara zaidi na hata kifo.

 Aina za Ectopic Pregnancy

Kuna aina kuu nne za mimba zinazotunga nje ya mfuko wa uzazi, nazo ni;

  1. Mimba zinazotunga kwenye mirija ya Fallopian.
  2. Mimba zinazotunga nje ya Uterus na nje ya mirija ya Fallopian.
  3. Mimba zinazotunga ndani na nje ya Uterus kwa wakati mmoja.
  4. Mimba zinazojirudia kutunga nje ya mfuko wa uzazi.

 Kuna njia za kuepuka tatizo hili hivyo ni vIZURI ukafuatilia makala haya.

Mimba kutunga nje ya mfuko wa uzazi wa mwanamke au Ectopic Pregnancy ni tatizo ambalo limetokea kuathiri wanawake mbalimbali. Kwa kawaida, isipokuwa mara chache sana, mimba zitungazo nje ya mfuko wa uzazi hazina uwezo wa kukua kuwa mtoto kamili.

Aidha, mimba hizi ni hatari kwa afya ya mama mjamzito kwa vile humfanya kupoteza damu nyingi na hatimaye kusababisha kifo. Baada ya utangulizi huo tulia angalia aina za mimba zinazotungwa nje ya mfuko wa uzazi.

Leo tutachambua aina hizo na sababu zake. Mimba zinazotunga kwenye mirija ya fallopian. Sababu kubwa inayopelekea mimba kutunga kwenye mirija ya fallopian ni kushindwa kusafirishwa kwa kiinitete katika mirija hii hali inayotokana na mabadiliko katika hali ya mirija au uwezo duni wa mirija hiyo katika kusukuma kiinitete kuingia kwenye uterus kwa sababu ya ukosefu wa vinyweleo kutokana na magonjwa mbalimbali yanayoathiri muundo na maumbile ya mirija ya fallopian.

Mimba zinazotunga kwenye mirija ya fallopian huwa zina madhara makubwa zaidi kwa sababu eneo hili ni jembamba mno kuweza kuhimili ukuaji wa mimba na pia lina mishipa mingi ya damu inayopita karibu ambayo ipo hatarini kupasuka hivyo kupelekea mgonjwa kupoteza damu nyingi sana.

Mimba zinazotunga nje ya uterus na nje mirija ya fallopian

Baadhi ya mimba huweza kutunga kwenye kiwanda cha kuzalisha mayai (ovary), kwenye shingo ya uzazi (cervix) au ndani ya tumbo (intra-abdominal). Aina hii ya mimba ni chini ya asilimia  tano ya mimba zote zinazotunga nje ya mfuko wa uzazi.

Mimba inayotungwa ndani ya tumbo (intra-abdominal) wakati fulani huweza kutoa mtoto aliye  hai tofauti na aina nyingine za mimba zinazotunga nje ya uterus. Hata hivyo uzalishaji wake  hufanywa kwa operesheni ingawa hakuna ushahidi wa kitabibu kuhusu suala hili mpaka sasa.

Madhara ya kutokea kwa upotezaji wa damu pamoja na maambukizi ni makubwa hivyo mara nyingi mimba za namna hii huitaji kushughulikiwa haraka ili kumuepushia madhara makubwa  mama mjamzito.

Mimba zinazotunga ndani na nje ya uterus kwa wakati mmoja Wakati fulani, mayai mawili yaliyorutubishwa kwa wakati mmoja hutokea kupandikizwa sehemu

mbili tofauti. Moja likipandikizwa nje ya uterus na jingine ndani ya uterus. Katika aina hii ya •  ectopic pregnancy, uwezekano wa yai lililotungwa ndani ya uterus kukua na kutoa mtoto ni  mkubwa sana.

Mimba zinazojirudia kutunga nje ya mfuko wa Uzazi

Wakati fulani hutokea kuwa, hata baada ya operesheni ya kuondoa mimba iliyotunga nje ya  kizazi kufanyika, baada ya muda fulani seli za kiinitete huendelea kukua na kujitengeneza tena  kufanya kusanyiko la seli kama mimba nyingine. Hali hii huitwa mimba zinazoendelea kutunga

nje ya mfuko wa uzazi au persistent ectopic pregnancy.

Kuna njia za kuepuka tatizo hili hivyo ni vema ukafuatilia makala haya nikukumbushe

kuwa Sigwa herbal clinic ni mabingwa wa kutatua matatizo mbalimbali katika mfumo wa

uzazi wa Mwanamke na mwanaume unaweza ukawatembelea katika vituo vyao. Bukoba,

Njombe, Singida, Dar es salaam, Moshi, Tanga, Mwanza, Mbeya, Arusha, Kahama, Kigoma, Dodoma na Morogoro.

Usikose kufuatilia mada hii Alhamisi ijayo kwenye gazeti hilihili.


Loading...

Toa comment