Unajua kwa nini mimba inatunga nje ya kizazi?-3

PainDuringpregnancyWiki iliyopita nilielezea sababu zinazofanya mimba itunge nje ya mfuko wa uzazi na kuzitaja. Leo naendelea na mada hii ili wasomaji wangu wapate kujifunza zaidi…

Aidha, mimba hizi ni hatari kwa afya ya mama mjamzito kwa vile humfanya kupoteza damu nyingi na hatimaye kusababisha kifo. Baada ya utangulizi huo tulia angalia aina za mimba zinazotungwa nje ya mfuko wa uzazi.

Leo tutachambua aina hizo na sababu zake.

Mimba zinazotunga kwenye mirija ya fallopian. Sababu kubwa inayosababisha mimba kutunga kwenye mirija ya fallopian. ni kushindwa kusafirishwa kwa kiinitete katika mirija hii hali inayotokana na mabadiliko katika hali ya mirija au uwezo duni wa mirija hiyo katika kusukuma kiinitete kuingia kwenye uterus kwa sababu ya ukosefu wa vinyweleo kutokana na magonjwa mbalimbali yanayoathiri muundo na maumbile ya mirija ya fallopian.

Mimba zinazotunga kwenye mirija ya fallopian huwa zina madhara makubwa zaidi kwa sababu eneo hili ni jembamba mno kuweza kuhimili ukuaji wa mimba na pia lina mishipa mingi ya damu inayopita karibu ambayo ipo hatarini kupasuka hivyo kusababisha mgonjwa kupoteza damu nyingi sana.

Mimba zinazotunga nje ya Uterus na nje ya mirija ya Fallopian.

Baadhi ya mimba huweza kutunga kwenye kiwanda cha kuzalisha mayai ovary, kwenye shingo ya uzazi Cervix au ndani ya tumbo Intra-Abdominal. Aina hii ya mimba ni chini ya asilimia tano ya mimba zote zinazotunga nje ya mfuko wa uzazi.

Mimba inayotungwa ndani ya tumbo Intra-Abdominal wakati fulani huweza kutoa mtoto aliye hai tofauti na aina nyingine za mimba zinazotunga nje ya Uterus. Hata hivyo, uzalishaji wake hufanywa kwa operesheni ingawa hakuna ushahidi wa kitabibu kuhusu suala hili mpaka sasa.

Madhara ya kutokea kwa upotezaji wa damu pamoja na maambukizi ni makubwa hivyo mara nyingi mimba za namna hii huhitaji kushughulikiwa haraka ili kumuepushia madhara makubwa mama mjamzito.

Mimba zinazotunga ndani na nje ya Uterus kwa wakati mmoja wakati fulani, mayai mawili yaliyorutubishwa kwa wakati mmoja hutokea kupandikizwa sehemu mbili tofauti.

Usikose kufuatilia mada hii Alhamisi ijayo kwenye gazeti hilihili.

Toa comment