#DALILI 10 ZA VIDONDA VYA TUMBO (ULCERS) NA MADHARA YAKE VISIPOTIBIWA
0717172230
✍🏻Vidonda vya tumbo ni tatizo linalotokea baada ya kuta za tumbo au utumbo mdogo kuwa na vidonda, hii hutokea ni baada ya kuharibika kwa ukuta wenye ute unaozuia kemikali za kuyeyusha chakula unaoitwa mucus.
✍🏻Kemikali ambayo ni acidi inayozalishwa mwilini kiasili husaidia kuyeyusha chakula na kuua wadudu tumboni, kama ukuta wenye ute ukiharibiwa na kushindwa kufanya kazi basi kemikali (acid) itaathiri tumbo au utumbo na kuruhusu bakteria kuendelea kusababisha vidonda vya tumbo.
✍🏻Vidonda vya mfumo wa umeng’anyaji chakula vikiwa kwenye tumbo tunaita vidonda vya tumbo ‘Gastric ulcer’, vikiwa katika duodenum tunaita ‘Duodenal ulcer’ na vikiwa katika esophagus tunaita ‘Esophageal ulcer’
✍🏻Vidonda vya utumbo mdogo (Duodenal ulcers)
✍🏻Hivi ni vidonda ambavyo hutokea kwenye utumbo mdogo (hasa juu)
CHANZO CHA VIDONDA VYA TUMBO
✍🏻Vidonda vya tumbo vina vyanzo tofauti ili vyote ni vile vinavyohusiana na mmeng’enyo, vyanzo hivyo ni;
1️⃣Bakteria waitwao Helicobacter pylori (H. pylori)
2️⃣Matumizi ya dawa za kupunguza maumivu kama asprin, (NSAIDs), (Advil, Aleve, na zingine)
3️⃣Kuwa na mawazo mengi
4️⃣Kula vyakula vinavyozalisha acid kwa wingi
4️⃣Kunywa pombe na vinywaji vikali
5️⃣Uvutaji wa sigara
6️⃣Kuto kula mlo kwa mpangilio
7️⃣Non-Steroidal Anti Inflammatory Drugs ‘NSAIDs’ ndio visababishi vikuu.
✍🏻Bakteria H.pylori wanahusika sana kwa angalau nne ya tano ya vidonda vya tumbo ‘Gastric ulcers’ & 95% ya ‘Duodenal ulcers’ ambapo NSAIDs husababisha 20% ya ‘Gastric ulcers’ na 5% ya ‘Duodenal ulcers’
✍🏻Bakteria H.pylori husababisha kupitia vyakula na maji. Pia hupatikana kwenye mate ya binadamu hivyo inaweza kusambazwa mdomo kwa mdomo wakati mkila denda/kunyonyana midomo.
✍🏻Bakteria H.pylori huishi kwenye kuta za utumbo na hutengeneza vimeng’enya ‘Enzyme’ iitwayo ‘Urease’ inayopunguza athari za asidi kwenye utumbo.
✍🏻Utumbo hutaka kufidia kiasi cha asidi kinachopotea kwa kutengeneza zaidi na husababisha kukwangua kuta za utumbo.
✍🏻Non-Steroidal Anti Inflammantory Drugs ‘NSAIDs’ ni dawa za kutuliza maumivu ya kichwa, maumivu ya hedhi, kushusha homa na kuondoa maumivu madogo madogo mfano Aspirin, Ibuprofen,Diclofenac & Meloxicam.
✍🏻Dawa hizi hupunguza uwezo wa kuta za tumbo na kufanya uwe rahisi kushambuliwa na asidi za tumboni hivyo kusababisha vidonda.
DALILI ZA VIDONDA VYA TUMBO
✍🏻Dalili za vidonda vya tumbo hujitokeza baada ya kula au kabla ya kula, ila mara nyingi wengi huwa wanazipuuzia na endelea kukuza tatizo, vidonda vya tumbo vinadalili kama;
1️⃣Kupata maumivu ya tumbo yanayokuwa kama ya moto (kuunguza) baada na kabla ya kula
2️⃣Kupatwa na kiungulia karibu na chembe ya moyo
3️⃣Tumbo kujaa gesi na kuvimbiwa
4️⃣Kichefuchefu na kutapika tena yawezekana kutapika damu
5️⃣Kupata haja kubwa ya rangi kahawia au nyeusi yenye harufu mbaya sana, pia haja yaweza kuchanganyikana na damu
6️⃣Kupoteza hamu ya kula na kupungua uzito
7️⃣Kushindwa kupumua vizuri
8️⃣Kuuma mgongo au kiuno
9️⃣Kupungukiwa au kupoteza kabisa nguvu za kijinsia
🔟Kukosa usingizi
✍🏻Nyingine ni kama;
➡️Maumivu makali sehemu ya mwili
➡️Kifua kwa ndani kana kwamba unachomwa na kitu cha moto au chenye ncha kali. Maumivu hayo wakati mwingine hutokeza mgongoni na huchoma kama sindano yenye sumu na kuacha maumivu makali
➡️Maumivu makali sehemu kilipo kidonda
➡️Kukosa choo au kupata choo kwa shida tena kikiwa kigumu na chenye kukatika kama cha mbuzi
➡️Kutapika nyongo
➡️Kutapika damu au kuharisha
➡️Sehemu za mwili kupata ganzi
➡️Kukosa hamu ya kula
➡️Kula kupita kiasi
➡️Kusahahu sahau na
➡️Hasira bila sababu.
✍🏻Hizo ni baadhi ya dalili za vidonda vya tumbo. Sio zote zilizotajwa hasa kwa mwenye vidonda sugu kwani hakuna hata kiungo kimoja mwilini atakachokuambia ni kizima.
JINSI YA KUEPUKANA NA VIDONDA VYA TUMBO
➡️Kunywa maji mengi
➡️Punguza mawazo, fanya mazoezi yatakupunguza na mawazo
➡️Punguza (balansi) kiwango cha halemu (choresterol)
➡️Usivute sigara
➡️Punguza au acha kunywa pombe
➡️Kula vizuri vyakula bora hasa asilia na sio vyakula vyenye kemikali
➡️Lala vizuri
Kama unasumbuliwa na vidonda vya tumbo wasiliana nasi kwa matibabu ya uhakika:
WhatsApp/phone 0717172230