The House of Favourite Newspapers

Unataka ajira ya uandishi, uhasibu benki, manunuzi na ugavi?

0

sda2134 033Baada ya jopo la wataalamu wa Chuo cha Mlimani Schoool of Professional Studies (MSPS) cha jijini Dar es Salaam, kugundua sababu zinazowafanya wahitimu wengi wa vyuo vikuu kukosa ajira nchini, chuo hicho kimepata muarobaini wa tatizo hilo.

Mkurugenzi wa chuo hicho kinachofundisha taaluma mbalimbali, Hassan Ngoma anasema katika mahojiano maalumu na gazeti hili kuwa chuo chao kimelazimika kubadili mfumo wa ufundishaji ili kwenda sambamba na mahitaji ya soko la ajira kwa wahitimu.

“Kelele za ukosefu wa ajira ni nyingi sana nchini; lakini ni kweli hakuna ajira kwa kiwango hiki tunachoambiwa? Jibu ni hapana, ukweli ni kwamba wasomi wetu wengi hawaajiriki.

“Juzi nilikutana na rafiki yangu ana kampuni kubwa tu, anahitaji watu wa kuajiri  lakini wenye sifa za kuajiriwa hakuna, wasomi tunaozalisha kwenye vyuo vyetu hawakidhi matakwa ya waajiri ndiyo maana utaona hata wakipata hizo ajira hawazitendei haki, wanaishia kufukuzwa.

“Sisi MSPS tumeamua kubadili gia ya ufundishaji, tunataka kuwa chuo tofauti na vingine, tunahitaji kutoa wahitimu wenye uwezo wa kufanya kazi, wenye ujuzi wa kuitumikia jamii, wahitimu ambao watakwenda kwenye kampuni kufanya kazi siyo kufundishwa kazi kama ilivyo sasa.

“Uchunguzi wetu umetufikisha mahali ambapo tutawafanya wanafunzi wanaosoma chuoni kwetu kutoka na elimu ambayo itakwenda kuwa lulu kwa kampuni, idara, viwanda na taasisi zote.

“Kama ni mwandishi, akihitimu chuoni kwetu atakwenda kwenye vyombo vya habari na kuwaambia wamiliki ‘nipeni nafasi ya majaribio niongeze tija ya kampuni kwa sababu nina mawazo haya, nikishindwa nitaondoka mwenyewe, sitaki mnilipe.”
“Mwandishi huyu akionesha mageuzi ya taaluma kwenye chombo alichokwenda kufanya majaribio, bila shaka ataajiriwa kwa sababu hakuna mmiliki wa chombo cha habari asiyetaka kampuni yake ipige hatua.

“Huu ndiyo motto wetu mpya wa ufundishaji tunaokuja nao hivi sasa, si kwa taaluma moja bali zote tunazotoa MSPS. Naomba wanafunzi wa kidato cha nne waliokosa nafasi za kuendelea na masomo waje chuoni kwetu wajisajili, nawahakikishia hawatapata shida ya kupata ajira ndani na nje ya nchi.

“Chuo chetu kimesajiliwa na NACTE kwa namba REG/BMG/036. Tunafundisha kozi mbalimbali kwa ngazi ya cheti na diploma ambazo ni; Business Administration, Banking and Finance, Human Resources Management, Procurement and Supply, Accountancy, Information Technology na Journalism and Mass Communication.
“Mpango huu wa mageuzi ya utoaji elimu inayokidhi matakwa ya waajiri utaanza Machi, 2016. Kuhusu mazingira ya chuo ni mazuri, hosteli zipo za kutosha kwa wanafunzi wa kutoka mikoani. Wale ambao wangependa kupata maelezo ya ziada wafike chuoni kwetu au tuwasiliane kwa namba za simu 0715-200900.

“Jambo la mwisho ambalo ningependa kulisisitiza ni kwamba chuo chetu hakijiendeshi kwa kutafuta faida kubwa, tupo kwa ajili ya kusaidia jamii, hivyo ada zetu ni nafuu sana na hutolewa kwa awamu tena kwa maelewano maalum.
“Wanafunzi waliokosa nafasi ya kuendelea na masomo hawana sababu ya kukosa fursa hii adimu katika nchi yetu ambapo mbali na kupewa elimu na uhakika wa ajira, bado wanafunzi wetu watapata nafasi ya kufundishwa na waandishi wa habari wazoefu, wahasibu wabobezi na wanataaluma mbalimbali nguli nchini wakiwemo wajasiliamali maarufu.

Leave A Reply