The House of Favourite Newspapers

Unataka kujiunga na freemasonry?

4

TedHoldCelebratesfiftyyearsinfreemasonry021.jpgHakuna ubishi kuwa historia ya kitu chochote ni mwalimu mzuri katika maisha yetu ya kila siku. Ukishajua historia ya jambo, itakutoa kwenye giza la usichokijua. Katika matoleo zaidi ya kumi kwenye safu hii, nimeeleza kwa kina historia ya Freemasonry ambayo ni jamii ya siri inayofanya mambo yake kwa siri huku ikihusishwa na mambo kibao ikiwemo imani ya kishetani na upatikanaji wa utajiri wa haraka.

HY17FREEMASONS_1397607fWiki iliyopita niliishia pale nilipokuwa nikizungumzia namna ambavyo hujishughulisha na masuala yote yanayohusu ustawi wa mwanadamu, kuhamasisha jamii kuwa na hisia za ukarimu na mapenzi mema kwa wanadamu wote, ikiwa ni pamoja na kutafsiri kanuni tunazojifunza na kuwa na ushawishi kivitendo.

SASA ENDELEA…

Rekodi za Freemasons katika Kabrasha la Greek Masonic zinaonesha kuwa lodges (majumba) kadhaa zilivyoundwa kama nilivyoeleza matoleo yaliyopita, mfano; Uingereza (mwaka 1717), Ireland (mwaka 1725), Ufaransa (mwaka 1728), Marekani (mwaka 1730) na Scotland (mwaka 1736), ndani yake utakuwa unajifunza ‘maandiko yao matakatifu’ na mwishowe utagundua na kuona yakiwa hai kwako na watu halisi na kufanikiwa kwao au kushindwa kwao. Utajifunza kuhusu kweli za Kibiblia na Fundi (Masoni) Mkuu wa Ulimwengu wanayemuita bwana wao yaani Master.

Narudia tena, kujiunga na Freemasonry ni hiyari yako na unaweza kujiunga kama unapenda kwa kutaka kwako mwenyewe. Lakini ifahamike kwamba si kila mtu anajiunga mwenyewe kwa kutaka.

Inawezekana pia ukawa umealikwa kwenye majumba yao kama mgeni lakini utachunguzwa na utaangaliwa kwa kina historia yako kisha utapewa kadi au utapigiwa kura na ndugu walio katika lodge (jumba) husika.

Kama ukitaka kujiunga na Freemasonry utalazimika kujifunza siri za ndani za majumba yao. Ni kweli ndani yake utajifunza lakini itategemea na kile unachokitaka kutoka kwao (wapo wanaotaka utajiri, umaarufu, uongozi au kukubalika tu kwenye jamii). Itategemea wewe unataka nini.

Baadhi ya siri za Freemasons ni pamoja na kushika namba za siri, ishara za maonyo na ishara za kiibada za kipekee. Utajifunza namna ya kutoa mikono au kupunga mikono kwa Kifreemason kupitia alama zinazoelekezwa katika ‘vitabu vyao vitakatifu’ vilivyoko kote duniani kama kitabu chao kiitwacho Old Charges.

Ndani ya kitabu hicho utakutana na maandiko ya zamani sana. Kingine ni Old Lodge Characters ambacho kina wakati wa nyuma zaidi ya mwaka 1390 na vitabu vya Freemasons kwa jumla.

Inaelezwa kwamba, kama unataka kuwa mwanachama wa Freemasonry, njia rahisi kujifunza kuhusu Freemasons na mambo yao, ni kusoma habari zao kwenye mitandao na vitabu vyao.

Kama ukijiunga nao, utaungana nao kurithi sherehe kubwa ambazo ziliadhimishwa tangu zamani kwa kukutana kwenye mahekalu yao na kumbi mbalimbali na anuani zao zinapatikana katika vitabu vya simu kama vya Marekani.

Ingawa unaweza kupiga simu ikawa ngumu kupokelewa kwa sababu hukutana mara mbili tu kwa mwezi na huwa hawataki mawasiliano ya mara kwa mara.

Kwa msingi huo, unaweza usimpate mtu unapopiga simu. Kuna taarifa kuwa Freemasons wengi hujivunia kuvaa pete na cheni maalum za Kimasoni hivyo kama unafikiria kujiunga nao ili uwe Master Mason, itakuwa manufaa kwako kama utajifunza sababu za kwa nini uvae pete za Kimasoni au alama zenye logo za Freemasons zenye pembe au kompasi.

Freemasons wengi huweka alama za Freemasony katika magari yao. Yaani stika zinazowahusu ili kuwa mtu fulani kwenye jamii.

Kuna swali nimekuwa nikiulizwa mara nyingi kama Freemasonry ni dini au inapingana na Dini ya Kikristo? Kama nilivyoeleza awali, Freemasons huwaalika watu wa kila dini na wana wanachama wa dini zote au kutoka katika dini zote ulimwenguni.

JIUNGE NA GLOBAL BRAKING NEWS UPATE HABARI KEMKEM ZA UCHAGUZI MKUU

globalbreakingnews.JPG

4 Comments
  1. juma says

    Mashaliti Yako Vipi

  2. muyuga says

    Nataka kujiunga nao naomba msaada

  3. MICHAEL MUTUA says

    Your Comment NATAKA KUJIUNGA NAO PLZ

  4. MICHAEL MUTUA says

    Your Comment NATAKA KUJIUNGA NAO PLZ PLZ!!

Leave A Reply