The House of Favourite Newspapers

Unataka Kurudiana Naye? Vizuri Ukayafahamu Haya-2

NI matumaini yangu msomaji uko poa, na­kukaribisha tena jam­vini tuangalie sehemu ya pili ya mada yetu. Wiki iliyopita tulijadiliana kwa kina kuhu­su suala la kuachana kisha kurudiana kwa watu ambao wapo kwenye uhusiano wa ki­mapenzi.

 

Pia tukatazama hasara au athari wanazoweza kukumbana watu wanaoishi kwenye aina hii ya uhu­siano. Nimepata meseji na simu nyingi kutoka kwa wasomaji wao, kila mmoja akielezea maoni yake na wengine wakinipa mikasa yao. Si vibaya kama nitakushirikisha mso­maji wangu kuhusu mkasa uliom­pata huyu ndugu yetu:

 

“Naitwa Halima wa Dar. Makala yako imenigusa na kusababisha nilie sana. Niliolewa miaka minne iliyopita na kubahatika kupata wa­toto wawili, wa mwisho ana umri wa miezi nane.

“Mume wangu aliniacha kwa ta­laka wakati mtoto akiwa na miezi mitatu tu na kwenda kwa mwan­amke mwingine. Kinachoniumiza ni kwamba mume wangu ameondoka katika kipindi ambacho bado nam­penda sana, kula sili wala usingizi sipati kila nikimfikiria.

 

“Kibaya zaidi ananita­mbia kwamba amem­pata mwanake anayemridhisha kuliko mimi na wakati mwingine nikimpigia simu anampa mwan­amke wake apokee. Natamani kurudiana naye kwa sababu bado nampenda na wanangu wanamhitaji lakini mwenyewe anaonesha hayupo tayari, ni­saidie nifanyeje?”

 

Hayo yalikuwa ni maelezo ya mso­maji wangu akiomba msaada wa ushauri kuhusu mada yetu tuliyoi­anza wiki iliyopita. Kama ungepata nafasi ya kumshauri dada Salama, ungemwambia nini? Tuma ushauri wako kupitia namba za hapo juu na utamfikia.

 

FAIDA ZAKE

Narudia kusisitiza kwamba japokuwa wengi wanaona kama ni jambo la ajabu kurudiana na mtu uliyekuwa unampenda, ni jambo la kawaida kabisa na watu wengi wa­nafanya hivyo duniani kote.

 

Takwimu zikionesha kwamba wanandoa au wapenzi waliowahi kupitia kipindi cha kutengana ki­sha wakarudiana tena, wana na­fasi kubwa ya kudumu kwenye uhu­siano wao kwa kipindi kirefu zaidi. Zifuatazo ni faida za kuachana na kurudi­ana:

  1. TAYARI MNA­JUANA: Mara nyingi un­apoanzisha uhusiano mpya, unaweza kudhani kwamba unampenda sana mtu uliy­enaye kwa sababu bado humfahamu kwa kina la­kini ukishamjua kwa un­dani, hasa tabia zake, yale mapenzi uliyokuwa nayo huisha haraka kwa sababu ya upun­gufu utakaoubaini. Unaporudiana na mwenzi wako, huanzi upya kwa sababu kama ni kumjua tayari un­amjua na yeye anakujua, unaelewa udhaifu na uimara wake, hali kad­halika na yeye anakujua kwa hiyo mkiamua kuwa ‘serious’, kazi in­

akuwa nyepesi kuliko kuanza upya na mtu mwingine.

  1. MMESHAKOMAA KIHISIA: Uamuzi wa kumrudia mtu aliyewahi kukuumiza, huhi­taji ujasiri mkubwa sana na ukiona umeweza kumsamehe na moyo wako bado unamhi­taji, hiyo ni ishara ya ukomavu wa kihisia. Kama mkirudiana pamoja, hakuna tena jambo linaloweza kuwasumbua kwa sababu mmeshapitia milima na mabonde.
  2. UMESHAJUA UMUHIMU WAKE: Kuna msemo mmoja maarufu kwamba huwezi kuo­na umuhimu wa kitu mpaka utakapokipoteza. Muda am­bao mmeachana, kila mtu hupitia kipindi kigumu kihisia. Huu ndiyo muda ambao un­aweza kupima kati ya mazuri na ma­baya ya mwenzi wako, yapi yalikuwa mengi.

Ukiona moyo wako bado unam­hitaji hata kama yapo aliyokuko­sea, tafsiri yake ni kwamba umeona umuhimu wake na utakapopata na­fasi ya kurudiana naye utakuwa ma­kini usimpoteze tena.

  1. HISIA ZAKO ZIMETULIA: Inapo­tokea unakorofishana mara kwa mara na mwenzi wako, zile hisia tamu za mapenzi kati yenu hupotea kabisa na matokeo yake mnaishi ki­mazoea. Lakini inapotokea mmeten­gana na kila mmoja akaendelea na mambo yake, hisia hutulia na kurudi upya. Mnaporudi­ana kila mmoja anakuwa mpya kihisia hivyo mnakuwa na nafasi kubwa ya kudumu.
  2. HAKUNA CHA KUWAY­U M B I S H A TENA: Wahen­ga wanasema n a h o d h a mzuri wa meli hupimwa wakati bahari i m e c h a f u k a . Ikiwa mme­shapitia kwenye m a c h a f u k o makubwa yaliyo­sababisha mpaka mkaachana, wakati mwingine kwa vu­rugu kubwa, ni dha­hiri kwamba kila mmoja ameshapata uzoefu. Hata ikitokea mmeko­rofishana tena, hakuna atakayekuwa tayari kuo­na mnarudi kule mliko­toka hivyo mtamaliza vi­zuri tofauti zenu.

Tukutane wiki ijayo kwa mada nyingine.

Comments are closed.