Undani wa Wema Sepetu Kuzimia Ghafla Usiku

Wema Isaac Sepetu ‘Madam’

AFYA ya staa mkubwa Bongo, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ haiku sawa, Risasi Mchanganyiko lina undani wa matukio yake ya kuzimia ghafla. 

 

Usiku wa kuamkia Jumapili iliyopita Wema alianguka na kupoteza fahamu usiku wa manani akiwa kwenye sherehe yake ya kuzaliwa (private party) iliyofanyika nyumbani kwa dada yake, Nuru Sepetu maeneo ya Mbezi-Beach jijini Dar.

 

Achana na tatizo la kukondeana linalozungumzwa na wengi, Risasi linafahamu kwamba hii ni mara ya tatu kwa mwanadashosti huyo kuzimia katika siku za hivi karibuni. Kufuatia tukio hilo la Jumapili kulizuka taharuki kubwa kwa wageni mbalimbali waliofika nyumbani hapo.

 

Chanzo chetu makini kilisema kuwa, sherehe hiyo Wema alifanyiwa kwa kushtukizwa bila yeye kufahamu ambapo walioshiriki ni rafiki na ndugu wa karibu, jambo ambalo lilimfurahisha mno Wema na badaa ya kufurahi huku vinywaji vikiendelea ndipo lilipotokea tukio hilo la kusikitisha.

“Unajua Wema alikuwa na furaha iliyopitiliza na wakati wote hakupenda kukaa wala kufanya chochote, badala yake alikuwa akipita huku na huku kuzungumza na rafiki zake ndipo alipojisikia vibaya na kudondoka kisha kuzimia ambapo ilibidi akimbizwe hospitalini kwa huduma ya kwanza ambapo aligundulika alikuwa na presha ya kushuka,” alisema mpashaji huyo.

 

Chanzo hicho kiliendelea kusema kuwa, pamoja na kadhia hiyo, lakini bado watu waliendelea kuisherekea siku ya kuzaliwa ya staa huyo huku wakimiminia zawadi na muziki wa kufa mtu ukiendelea mpaka staa huyo alipopatiwa matibabu na kurejea nyumbani salama.

 

Hata hivyo, kipindi cha nyuma, Wema aliwahi kujisikia vibaya katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika kwenye ofisi za StarTimes jijini na kukimbizwa hospitalini kisha kugundulika ana presha ya kushuka.

STORI: IMELDA MTEMA  RISASI MCHANGANYIKO

Toa comment