The House of Favourite Newspapers

UNI INDUSTRIES YATANGAZA HABARI NJEMA KWA WAJASIRIAMALI


Katika kuunga mkono juhudi za mheshimiwa Rais Dokta John Pombe Magufuli za kuipeleka Tanzania katika uchumi wa kati wa viwanda, Kampuni ya Uni Industries imetangaza habari njema kwa wajasiriamali wadogo kwa wakubwa.

Kampuni hiyo inayohusika na uuzaji wa vifaa mbalimbali vya mahotelini, majumbani na viwanda vidogo, inaendelea kuuza vifaa bora kwa wajisiriamali kwa bei ambayo Mtanzania wa kawaida anaweza kuimudu na hivyo kujikwamua kiuchumi.

“Tunawasaidia wajasiriamali wanaofika kwenye maduka yetu kwa ajili ya kununua vifaa mbalimbali, kuwaelekeza namna ya kuvitumia vifaa hivyo kutengeneza faida kubwa ndani ya muda mfupi.
“Tunauza vifaa bora kwa ajili ya huduma za cartering kwa wale wanaofikiria kuanzisha huduma za kusambaza vyakula kwenye shughuli mbalimbali kwa bei nafuu.

Lakini pia tunauza mashine za pop corn, mashine za kukamulia juisi, majiko ya kuokea mikate kwa wanaotaka kuanzisha biashara za bakery, majiko ya kupikia keki, mashine za kufulia nguo (laundry) kwa wanaotaka kuanzisha biashara za udobi na kadhalika.

“Bidhaa zetu zote zinatengenezwa kwa ubora wa kimataifa, tunavyo vifaa kutoka kwa washirika wetu, MacAdams, IPSO, Foodserv Solutions na kadhalika, yanayosifika kwa kutengeneza bidhaa zenye ubora wa hali ya juu duniani kote kwa hiyo mjasiriamali atakuwa na uhakika na fedha zake anazotoa na pia atapewa elimu ya kutosha kuhusu biashara anayotaka kuianzisha.

“Maduka ya Uni Industries pia yamesambaa kuanzia hapa jijini Dar es Salaam, Zanzibar, Kenya, Uganda na Rwanda na hii ni uthibitisho mwingine kwamba ubora wetu ni wa kimataifa.
“Mbali na vifaa vya wajasiriamali, pia tunavyo vifaa vingine kwa ajili ya wenye mahoteli makubwa na vya majumbani kwa bei poa kabisa ambapo mteja anaponunua, anakuwa na uhakika wa fedha zake kwa kipindi kirefu.

Kwa mahitaji ya vifaa vingine vingi vya kisasa, tembelea maduka ya Uni Industries yaliyopo Staywell Complex, plot 1720, Haile Sellasie Road, mkabala na Marrybrown, Namanga jijini Dar es Salaam na Forodhani, Zanzibar.

Pia unaweza kuwasiliana nao kwa simu namba 0681 111 999 au 0766 075 031 au kwa barua pepe [email protected]. Pia unaweza kutembea website yao kwa kubofya www.uni-eastafrica.com. Wahi sasa ili uwe miongoni mwa watu wanaokwenda na wakati kwa kumiliki vifaa vya kisasa vyenye teknolojia ya hali ya juu.

Comments are closed.