POLISI Mkoa wa Mwanza imefanikiwa kumuokoa mtoto mchanga wa kiume anayekadiriwa kuwa na umri wa siku moja hadi tatu aliyekuwa ametupwa na mtu asiyefahamika katika Mtaa wa Mwambani, wilayani Ilemela.
Tukio hilo la kikatili limetokea tarehe 17.12.2018 majira ya saa 2:30 usiku, baada ya mtoto huyo kufungwa nguo mwilini kisha kutupwa. Polisi waliokuwa doria walipata taarifa na kufika eneo husika na kumkuta mtoto huyo akiwa hai huku akilia.
Mtoto huyo alipelekwa Hospitali ya Rufaa ya Bugando kwa ajili ya matibabu na uhifadhi ambapo hali yake inaendelea vizuri.
Jeshi hilo linasaka mhusika ili afikishwe katika vyombo vya sheria.
Aidha, polisi imetoa onyo kwa watu wenye tabia hii ambalo ni ni kosa la jinai na ni kinyume na haki za binadamu. Pia imewaomba wananchi pindi wanapomwona mjamzito ambaye ujauzito wake hupotea na mtoto haonekani, watoe taarifa polisi ili wachukua hatua za kujiridhisha juu ya usalama wa mtoto.
Comments are closed.