The House of Favourite Newspapers

Updates: Hukumu ya Sugu Mahakani Mbeya

Mahakama ya Hakimu Makazi Mbeya leo inatarajia kutoa hukumu ya kesi ya kumkashifu Rais Dkt. Jonh Magufuli inayowakabili Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi na Katibu wa CHADEMA Nyanda ya Juu Kusini, Emmanuel Masonga.

Watuhumiwa ambao ni Sugu na Masonga tayari wameshafika mahakamani hapo huku ulinzi ukiwa umeimarishwa katika eneo la Mahakama.

Wengine ambao tayari wameshafika mahakamani hapo ni makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Profesa Abdallah SafariNaibu Katibu Mkuu wa Chadema Bara, John Mnyika, mke wa Sugu na wengine.

Tayari Sugu na Masonga wameingia ndani ya mahakam hiyo na kesi hukumu yao imeshaanza kusikilizwa.

Washtakiwa wanadaiwa kutenda kosa hilo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Desemba 30,2017 eneo la Uwanja wa Shule ya Msingi Mwenge jijini Mbeya. Hakimu Mkazi Mfawidhi, Michael Mteite anatarajiwa kutoa hukumu baada ya upande wa mashtaka na ule wa utetezi kukamilisha ushahidi Februari 9, 2018.

Upande wa Jamhuri iuiwasilisha mashahidi watano na kielelezo kimoja cha sauti iliyodaiwa kurekodiwa na shahidi wa tano, Inspekta Joram Magova. Upande wa utetezi uliwasilisha mashahidi sita wakiwamo Sugu na Masonga waliokana kutamka maneno wanayoshtakiwa kuyatoa.
Washtakiwa walitetewa na mawakili Sabina Yongo, Boniface Mwabukusi na Hekima Mwasipu kabla ya kujitoa na sasa wanawakilishwa na Peter Kibatala na Prof Safari. Sugu na Masonga  walifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza, Januari 16 na kusomewa mashtaka na Wakili wa Serikali Mkuu, Joseph Pande aliyeeleza upelelezi ulikuwa umekamilika na walikuwa tayari kuendelea na usikilizaji.

BREAKING! Sugu Ahukumiwa Jela Miezi 5!

Comments are closed.