The House of Favourite Newspapers

Updates: Ndege ya Precision Air Yaanguka Bukoba, 26 Waokolewa Kati ya 43 -Video

0

 

Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Albert Chalamila amesema Ndege ya Precision Air iliyopata ajali wakati wa kutua Bukoba leo Jumapili Novemba 6, 2022 ilikuwa imebeba watu 43 ambapo hadi sasa wameokolewa 26 tu na kupelekwa Hospital ya Rufaa ya mkoa Kagera.

 

Japo Mkuu wa Mkoa hajasema watu hao waliokolewa vipi na muda gani, Mashuhuda wanasema huenda waliokolewa sekunde chache baada ya ajali kabla sehemu kubwa ya Ndege hiyo kufunikwa na maji, tunaendelea kufuatilia zaidi ili kupata taarifa kamili kutoka kwa Mamlaka.

 

Kwa upande mwingine RC Chalamila amewaomba Wananchi kuendelea kuwa watulivu maana mawasiliano na Marubani walioko ndani ya ndege bado yanaendelea.

 

Ndege hiyo ni ATR 42 yenye namba za usajili 5H BWF ambayo ilikua ikitokea Dar es salaam kuelekea Bukoba na ilikua na safari ya kurudi Dar es salaam kupitia Mwanza.

 

NDEGE YA PRECISION AIR YAANGUKA MJINI BUKOBA MKOA WA KAGERA

Habari zilizoifikia hivi punde asubuhi hii ya Jumapili Novemba 6, 2022 ni juu ya kuanguka kwa Ndege ya Shirika la Precision Air mjini Bukoba Mkoa wa Kagera.

Ndege hiyo inaonekana ikielea kwenye maji katika Ziwa Victoria ambapo watu wanaokolewa hivi sasa.

Global TV ipo eneo la tukio ambapo imeshuhudia ndege hiyo ikielea kwenye maji huku watu wakiokolewa.

Endelea kuwa nasi kupata mwendelezo wa habari hii.

Leave A Reply