The House of Favourite Newspapers

UPDATES YA AJALI: Waziri Kigwangalla Alazwa Kituo Cha Afya Magugu, Manyara

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akiwa amelazwa katika kituo cha afya Magugu akipatiwa matibabu.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla amelazwa katika kituo cha afya Magugu akipatiwa matibabu zaidi kutokana na majeraha aliyoyapata katika ajali asubuhi leo akitokea mkoani Arusha kuelekea Manyara karibu na eneo la Magugu ambapo Ofisa wa habari, Hamza Temba amefariki dunia.

Katika ajali hiyo ya gari kulikuwa na watu sita akiwamo Waziri Kigwangalla ambaye ameumia katika mbavu, mkono na shingo. Kwa sasa anaendelea vizuri baada ya kupatiwa matibabu wilayani Manyara ambapo  pia wakiandaa utaratibu wa kumhamishia yeye pamoja na majeruhi wengine katika hospitali kubwa kwa matibabu zaidi.

Comments are closed.