The House of Favourite Newspapers

FT: YANGA 1-1 PRISONS, UWANJA WA AZAM COMPLEX

0

Dakika ya 85: Yanga wanafanya mabadiliko, anatoka Ajibu anaingia Yusuph.

Dakika ya 79: Ibrahim Ajibu anapata kadi ya njano kutokana na kujiangusha ndani ya eneo la 18 la Prisons.

Dk ya 79: Ajibu anapewa kadi ya njano kwa kujiangusha ndani ya eneo la 18 la Prisons.

Dk ya 76: Fred Chudu wa Prisons yupo chini, ameumia, mchezo unasimama kwa muda, anatolewa nje kisha mchezo unaendelea.

Dakika ya 73: Yanga wanamtoa Emmanuel Martine, anaingia Geofrey Mwashiuya.
Dk ya 65: Yanga wanaanza kulisogelea lango la Prisons mara kadhaa.

Dk ya 60: Kasi ya mchezo imepungua, timu zote zinacheza kwa tahadhari.

Dakika ya 50: Yanga wanaanza kupanga mashambulizi.

Dakika ya 46: Mchezo umeanza kwa timu zote kusomana.

Kipindi cha pili kinaanza.

MAPUMZIKO

Mchezo sasa ni mapumziko.

Mwamuzi anakamilisha kipindi cha kwanza.

Dk ya 42: Yanga wanapata bao la kusawazisha mfungaji ni Raphael Daudi, kutokana na mpira wa kona iliyopigwa na Ibrahim Ajibu.

Dk ya 36: Lambati Sabiyanka anapata kadi nyekundu kutokana na kumchezea faulo Juma Abdul.

GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO

Dk ya 10: Prisons wanapata bao la kwanza mfungaji ni Eliuter Mpepo baada ya walinzi wa Yanga kufanya uzembe wakati wakimdhibiti.

GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO

Dk ya 8: Yanga wanaonekana kama bado hawajakaa sawa, Prisons

Mchezo umeanza.

Huu ni mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara unaochezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

Leave A Reply