The House of Favourite Newspapers

Upige Mwingi Na Airtel-Kila Mtu Ni Mshindi Ukiwa Na Airtel

0
Msanii wa Komedi na Balozi wa Airtel maarufu kwa jina la Joti akimvalisha fulana mmoa wa wateja wa Airtel kwenye Viwanja vya Zhakhiem ulipofanyika uzinduzi huo.

Dar es Salaam, Jumatano 3 Mei 2023: Kampuni ya mtandao wa simu za mkononi ya Airtel Tanzania inayoongoza kwa kutoa huduma bora za mawasiliano pamoja na huduma za kifedha kupitia simu za mkononi, leo imetangaza kuzindua promosheni mpya ijulikananyo kama ‘Upinge Mwingi na Airtel – Kila Mtu ni Mshindi’ ambayo  itawawezesha wateja na mawakala wake wote nchini kujishindia zawadi kabambe pale wanapotumia huduma au wanapofanya miamalan kwa kutumia Airtel Money.

Mkurugenzi wa Huduma za Airtel Money Tanzania, Andrew Rugamba akizungumza na umati uliofurika Viwanja vya Mbagala Zakhiem jijini Dar kushuhudia uzinduzi huo.

Hii ni promosheni ya kipekee kwani kila mteja au wakala wa Airtel ni mshindi, wateja na mawakala wataweza kujishindia zawadi za papo hapo kama vile muda wa maongezi , pikipiki, TV , Friji, na Fedha taslimu kuanzia shilingi milioni moja mpaka milioni hamsini za Kitanzania.

Si hivyo tu zaidi ya zawadi hizo pia Airtel imeongeza sababu nyingine ya kutabasamu kwa wateja wake kwani sasa kuangalkia salio la akaunti ya Airtel Money hakunja makato ni bure kwa wateja wote.

Joti akiuchekesha umati uliofurika Viwanja vya Mbagala Zakhiem kwenye uzinduzi huo.

Promosheni ya Upige Mwingi na Airtel itadumu kwa kipindi cha miezi mitatu ambapo kila mteja au wakala wa Airtel anaponunua bando au kufanya muamala wowote kwa kutumia Airtel Money kama vile kutuma fedha, kutoa fedha kuloipa bili au au Lipa namba atapata zawadi ya papohapo ya muda wa maongezi na vilevile kuingia kwenye droo ya kila siku, wiki nay a mwezi ili kujishindia zawadi.

Maofisa wa Airtel wakiwa kwenye picha ya pamoja na mchekeshaji Joti.

Mteja anayefanya miamala mingiu zaidi anayo nafasi kubwa ya kujishindia zawadi, mawakala wa Airtel Money nao wanayo nafasi ya kuingia kwenye droo na kujishindia zawadi pia.

Airtel kuanzia leo imeondoia makato ya kuangalia salio, mteja anaweza kupiga *150*60#au kutumia App ya Aitel, hakuna makato tena kuangalia salio. Airtel inakuwa kampuni ya kwanza nchini Tanzania kuondoa gharama za kuangalia salio la Airtel Money kwa wateja wake wote. Ukiwa na Airtel kila mtu ni mshindi!

Lengo la promosheni hii ni kuendelea kuwahamasisha wateja na mawakala kutumia huduma za Airtel na wakati huohuo kupata nafasi ya kujishindia na Airtel na kuweza kutimiza ndoto zao.

Kutakuwa na zawadi za kila siku ambapo washindi 90 watajishindia shilingi milioni moja, washindi 48 wa kila wiki watajishindia friji la milango miwilina TV yenye ukubwa wa inchi 55 , washindi wawili kujishindia pikipiki mpya kwenye droo ya mwezina mshindi kujishindia milioni 50 kwenye droo ya mwisho.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo wakati wa kuzindua promosheni hiyo ya Upige Mwingina Airtel – Kila mtu ni Mshindi, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania, Beatrice Singano alisema Upige Mwingi na Airtel ni promosheni ya kipekee ambapo kila mteja wa Airtel kuanzia sasa atapata zawadi kila atakapotumia huduma ya Airtel.

Kila mtu atajishindia zawadi ya muda wa maongezi papohapo pale atakapokuwa amefanya muamala wowote au kununua bando.

Naye Mkurugenzi wa Huduma za Airtel Money Tanzania, Andrew Rugamba aliongeza;

“Sisi Airtel tunajali na tumejitolea kuhudumia wateja wetu, Aitel Tanzania ilikuwa kampuni ya kwanza kuondoa tozo kwenye miamala ya simu kwa wateja wote na sasa ndiyo ya kwanza kuondoa gharama au makato ya kuangalia salio.

“Hii inaongeza thamani sana kwa wateja wetu kuokoa pesa na kukamilisha maana ya kila mteja wa Airtel Money kuwa mshindi. Alimaliza kusema.

Singano pia alielezea mipangfo ya Airtel kusambaza huduma zake kote nchini;

“Tumekuwa tukiendelea kupanua wigo wa mtandao wetu na mpaka sasa tuna matawi ya Airtel Money 3,500 na wakala 200,000 huku pia tukiendelea kuwekeza kwenye kupanua mtandao wa 4G ili kufikia Watanzania wotena hasa maeneo ya vijijini.

     

Leave A Reply