Uponyaji Kwa Wenye Shida Mbalimbali Waanza Kwa Kasi Buza Kwa Lulenge
Dar es Salaam, 23 Septemba 2024: Huduma za uponyaji kwa wenye shida mbalimbali zimeanza kwa kasi kwenye Kanisa la Bethlehem Gospel Revival chini ya Askofu Edward John lililopo Buza Kwa Lulenge jijini Dar ambapo zamani alikuwa akihudumu Pastor Dominic maarufu Kiboko ya Wachawi ambalo ni tofauti na kanisa lililopo hivi sasa.
Wanahabari wetu wakiwa kwenye ibada kanisani hapo jana Jumapili walishuhudia wenye shida mbalimbali wakiombewa masuala binafsi, wagonjwa na wenye mbalimbali.
Akizungumza na Mwanahabari wetu baada ya ibada hiyo, Askofu Edward amesema huduma za maombezi kanisani hapo ni kila siku ya Jumapili, Jumanne na Alhamisi kuwakaribisha wenye shida mbalimbali zinazohitaji maombi pamoja na ibada ya kumsifu na kumtukuza Bwana.