visa

Ureno Yafunga Akaunti za Benki za Bilionea Mwanamke Afrika.

Nchi ya Ureno imezifunga kwa muda akaunti zote za benki zilizo nchini humo za mwanamke tajiri zaidi barani Afrika, Isabel dos Santos.

Ureno wamepewa amri ya kufanya hivyo kutoka katika vyombo vya usalama vya nchini Angola, wakati ambao upelelezi wa kesi yake bado unaendelea.

Dos Santos ambaye ni  mtoto wa Rais wa zamani wa Angola Jose dos Santos, ameshtakiwa nchini Angola kwa tuhuma za ufisadi lakini yeye amepinga tuhuma hizo na kuziita siasa.
Toa comment