Urusi Yaripotiwa Kumuua Mwandishi wa Habari Raia wa Ukraine

Maks Levin mwandishi wa habari anayeripotiwa kuuawa na vikosi vya Urusi

MWANDISHI wa habari raia wa Ukraine anayefahamika kwa jina la Maks Levin ameripotiwa kuuawa na vikosi vya Urusi katika msitu nje kidogo ya Jiji la Kyiv.

 

Levin ambaye alikuwa ni mpiga picha aliyekuwa akifuatilia kwa karibu mauaji na unyanyasaji wa vikosi vya Urusi anadaiwa kufanya kazi na mashirika mengine ya habari kama vile Reuters na BBC na anaripotiwa kuuawa mnamo mwezi Machi mwaka huu na maiti yake kupatikana Aprili 1.

 

Shirika lisilokuwa la kiserikali la Utangazaji ambalo linafanya kazi ya kukusanya habari zake bila mipaka la RSF limeripoti kuwa lina ushahidi wa kuwa wanajeshi wa Urusi wametekeleza mauaji kwa mwandishi huyo wa habari.

 

Shirika hilo la RSF limeripoti kuwa lilituma wachunguzi wawili kwenda kuchunguza juu ya mauaji ya Levin na ripoti ilirudi ikibainisha kuwa Levin pamoja na mwenzake aliyeongozana naye alikuwa ameuawa.

 

“Ushahidi dhidi ya vikosi vya Urusi unatisha.” Kimesema chanzo hicho cha RSF

 

Tayari Shirika hilo la RSF limethibitisha kupeleka ushahidi wote kwenye Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Ukraine.

 

 2176
SWALI LA LEO

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?
Toa comment