USAGM/Voice of America Watoa Somo Kwa Washirika Wake wa Barani Afrika

Washiriki wa kongamano hilo wakiwa katika picha ya pamoja.

 

BODI ya Utangazaji ya Marekani (USAGM), Sauti ya Amerika (VOA) kwa kushirikiana na Shirika la Utangazaji la Global Press, wameendesha kongamano la namna bora ya kuimarisha vyombo vya habari kwa washirika wake wa barani Afrika, iliyofanyika jijini Cape Town nchini Afrika Kusini.

Baadhi ya washiriki wa kongamano hilo wakijifunza jambo.

 

Katika kongamano hilo la siku tatu lililomalizika leo, Juni 27, 2022, mada zilizotolewa ni pamoja na namna bora ya kuimarisha vyombo vya habari na kuweka kanuni madhubuti za kiusalama kwa waandishi wa habari.

 

Kutoka kulia ni Mr. Brenard kutoka Sychelles TV, Mr Abdallah Mrisho kutoka Global TV na Nasra kutoka Somali TV.

 

Viongozi wa washirika wote wa Sauti ya Amerika (VOA) kutoka vyombo vya habari vya Tanzania, Kenya, Uganda, Somalia, Sudani Kusini, Malawi, Zambia, Zimbabwe, Ethiopia, Seychelles na DRC wamehudhuria na kujifunza mbinu na kanuni mbalimbali za kutumia katika mazingira mbalimbali, bila kuhatarisha maisha ya waandishi wake.

 

Mmoja kati ya wakufunzi wa VOA, Travis Hayde kutoka Afrika Kusini akiwasilisha mada.

 

Kongamano hilo limeendeshwa na wakufunzi kutoka Global Press, @globalpressjournal (http://www.globalpress.co) shirika ambalo linaendeshwa na waandishi wa habari, wahariri wanawake, wakufunzi na wataalam wa kimataifa wa maendeleo likiwa na matawi mbalimbali barani Afrika, Amerika Kusini na Asia.3473
SWALI LA LEO

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?
Toa comment