The House of Favourite Newspapers

Usajili Bongo ni Mwendo wa Fedha Tu

0
Mwenyeki wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe (kulia) akiwa na Emmannuel Okwi.

HABARI ya mjini kwa sasa ni kuhusiana na usajili ambao unaendelea kufanywa na timu zote 16 zitakazoshiriki Ligi Kuu Bara kwa msimu ujao.

Kila kamati ya usajili ya timu husika ipo bize kuhangaika huku na kule kuvisuka vikosi vyao kwa kuzipata saini za wachezaji ambao wamewaweka kwenye mipango yao ili tu waje kuzibeba timu hizo msimu ukianza.

Licha ya dirisha la usajili kuwa na siku chache tangu lilipofunguliwa, lakini picha inaonyesha kuwa klabu zimetumia fedha nyingi kwa kufanya uhamisho wa wachezaji kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

 

Beki wa kushoto wa Azam FC, Gardiel Michael Mbaga amesaini mkataba wa awali wa miaka miwili kujiunga na Klabu ya Yanga.

Championi Jumatano, linakuchambulia juu ya fedha ambazo zimetumiwa na t i m u t a t u zenye kawaida ya kutumia s a n a f e d h a kwenye usajili ambazo ni Simba, Yanga na Azam.

SIMBA Yenyewe ndiyo timu ambayo imefanya usajili wa nyota wengi mpaka sasa. Ndani ya kikosi chao kuna sura mpya saba ambazo zimesajili w a kwen y e kipindi hiki cha usajili.

Klabu ya Singida United imekamilisha mchakato wa kumsajili beki Miraj Adam ambaye alikuwa akiichezea African Lyon msimu uliopita.

S i m b a imesajili nyota wengi kutokana na kikosi hicho kushiriki michuano ya kimataifa kwa msimu ujao, ambapo kwa makadirio ya fedha ambazo wamezimwaga kwenye usajili zinaweza kufi ka Sh milioni 200. Iko hivi, Simba wamewachukua ambao wamechota fedha za timu hiyo ni Emmanuel Mseja (Sh mil 25), Ally Shomari (Sh mil 20), Jamal Mwambeleko (Sh mil 15) na Yusuph Mlipili (Sh mil 20).

YANGA Bado haijawa na makeke yake ambayo yamezoeleka na wengi kinapofi ka kipindi hiki cha usajili, lakini tayari imeshafanya usajili za wachezaji kadhaa, akiwemo Ibrahim Ajibu wa Simba. Kikosi hiki kinachonolewa na Mzambia, George Lwandamina, kishawasajili wachezaji watano ambao wamechota kiasi cha Sh milioni 145.

Ibrahim Ajibu wa Simba.

Nyota waliokula fedha hizo ni Ajibu (Sh milioni 50), Abdallah Shaibu (Ninja) kutoka Taifa Jang’ombe ya Zanzibar (Sh mil 15), Pius Buswita wa Mbao (Sh mil 20), Gadiel Michael wa Azam FC (Sh milioni 20) na kipa Mcameroon, Ronstand Youthe aliyetia kibindoni Sh mil 40 akitokea African Lyon.

AZAM Kwa sasa wametambulisha sera mpya ndani ya kikosi chao ya kutotumia fedha nyingi kufanya usajili hasa kwa wachezaji wa kimataifa, kutokana na kutoona faida ya wachezaji hao kwa kushindwa kuipa mafanikio makubwa.

Japo wapo kwenye machungu ya kuondokewa na wachezaji wao watatu, John Bocco, Aishi Manula na Shomari Kapombe, lakini nao wamejitutumua na kufanya usajili wa wachezaji ambao wataziba mapengo ya wachezaji hao. Azam mpaka sasa ishatumia Sh milioni 95 kukisuka upya kikosi chao kwa kusajili wachezaji wanne, japo wapo kwenye mchakato wa kusajili zaidi na zaidi.

Waliochota kiasi hicho ni kipa mrithi wa Manula, Benedict Haule aliyetoka Mbao aliyechikichia mfukoni Sh milioni 15, kiungo, Salmin Hoza (Sh mil 20) na washambuliaji, Mbaraka Yusuph (Sh mil 40) na Wazir Junior (Sh mil 20). Ukiziondoa timu hizo tatu kumwaga fedha katika usajili huu, pia klabu kama Singida United ya Singida imekuwa ikimwaga fedha za kutisha kwa kufanya usajili wa wachezaji mbalimbali.

 

Singida ambayo imekuwa ikifi cha madau ambayo wanawapa wachezaji wao, mpaka sasa ishamalizana na Wazimbabwe, Twafadzwa Kutinyu, Elisha Muroiwa, Wisdom Mtasa, Nhivi Simbarashe, Mganda, Shafi k Batambuze pamoja na Mnyarwanda, Danny Usengimana. Pia wametumia milioni 20 kumpata kiungo Kenny Ally kutoka Mbeya City.

nyota wa A z a m , J o h n B o c c o , Shomari Kapombe na Aishi Manula ambao peke yao wameikamua timu hiyo milioni 120, Kapombe na Manula wamechukua Sh milioni 35 kila mmoja, huku Bocco akibeba Sh milioni 50.

MAKALA: SAID ALLY

Leave A Reply