The House of Favourite Newspapers

Yondani: Nyie Yanga, Tutakutana Ligi Kuu- Video

Beki wa kati wa Yanga, Kelvin Yondani.

BEKI wa kati wa Yanga, Kelvin Yondani, ame­vunja ukimya kwa kuwa­taka viongozi wa Yanga waache maneno ya kula­lamika na kumtengenezea lawama kwa wapenzi wa soka bali wampe fedha asaini, huku akisema wakigoma atacheza timu nyingine.

 

Yondani msimu uliopita alien­delea kuonyesha kiwango kizuri huku akitoa mchango mkubwa ndani ya kikosi hicho pamoja na kwamba awali alionekana kutokuwa vizuri.

 

Beki huyo kwa muda mrefu hasa kipindi hiki cha usajili, amekuwa akihusishwa na ku­jiunga na Simba.

Akizungumza na Championi Jumatano, Yondani amefun­guka kuwa tangu mkataba wake na Yanga ulipofikia tamati mwishoni mwa msimu uliopita viongozi wake wamekuwa waki­toa maneno tu badala ya fedha, jambo ambalo linamfedhehe­sha kwani yeye hachezi mpira kwa sifa tena zaidi ya kuangalia maisha yake ya baadaye.

 

“Ninashangazwa sana pale ninapoona viongozi wangu wanaongea mengi juu yangu wakati ukweli wa yote una­baki kwao, kuwa hadi sasa wameshindwa kunitimizia mahitaji yangu ya msingi ili niendelee kuitumikia Yanga.

“Kikubwa wao baada ya kumaliza mkataba wangu walipaswa kunipatia changu ili niwe na uhuru wa kufanya maamuzi mazito juu ya familia yangu, zaidi wamekua wakitoa porojo tu bila kufikia muafaka jambo ambalo si zuri kwani wanani­chonganisha na wapenzi wa soka ambao ukweli wa jambo hawaufahamu kuwa wao ndiyo kikwazo kwangu.

 

“Naomba itambulike kuwa umri wangu wa sasa hauon­gozwi na mapenzi ya timu tu bali unaongozwa zaidi na hali halisi ya maisha yangu ya nyumbani hivyo sipo kwa ajili ya kuiangalia Simba, Yanga na Azam tu zaidi ya fedha ambayo ndiyo mhimili wa kipaji changu.

 

“Ukimya wa viongozi wangu juu ya kunipa fedha ili nisaini mkataba mpya usiwafanye mashabiki wakadha­ni sitacheza msimu ukianza, kwani hata Yanga wakiendelea kuremba wao wajue tu kuwa tutakutana mwanzoni mwa msimu mpya nikicheza ligi hiihii maana timu zipo nyingi zilizozungumza na mimi na naelekea kuchoka kuwasubiria Yanga maana wanajifanya ha­watambui kama mpira ni pesa,” alisema Yondani bila ya kuitaja timu ambayo ataichezea baada ya kuondoka Yanga.

 

 

Comments are closed.