The House of Favourite Newspapers

USAJILI WA MANULA SIMBA BADO UTATA, SIKIA TAMKO LA BOSI WA AZAM

0
Aishi Manula.

Wakati kikosi cha Simba kikiendelea kufanya maandalizi ya msimu ujao wa 2017/18 nchini Afrika Kusini, upande mwingine bado kuna utata juu ya mchezaji Aishi Manula ambaye anatarajiwa kuitumikia timu hiyo katika msimu huo.

Inajulikana wazi kuwa Manula bado hajamaliza mkataba wa kuitumikia Azam FC lakini tayari ameshamalizana na Simba, hivyo hawezi kuanza majukumu yake mapya hadi mkataba wake utakapomalizika siku kadhaa zijazo.

Simba imekuwa ikihitaji kuanza kumtumia Manula lakini haiwezi kufanya hivyo kwa kuwa itakuwa imekiuka masharti ya mkataba.

Sasa, Mwenyekiti wa Idrisa Nassor ‘Father’ ametoa tamko kuwa Manula bado ni mchezaji wao na kuhusu masuala ya Simba kumsajili wao hawafahamu.

Nassor amesema kuwa licha ya kuwa Manula bado ni mchezaji wao kimkataba, lakini kuhusu kuendelea kuwa naye au kutomuongezea mkataba hilo ni suala tofauti na hawezi kulifafanua.

Leave A Reply