Ushauri wa wote amenitumia meseji niachane naye!

HABARI ya kazi anko. Naitwa Cecy wa Dar, naomba ushauri. Mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 22. Tatizo langu nilikuwa na mchumba lakini kwa bahati mbaya tulikorofishana lakini tulipatana. Mwisho wa siku akanitumia meseji niachane naye, anko nifanyeje ikiwa bado nampenda sana?

Jibu: Anayekutumia meseji ya kukwambia uachane naye, mara nyingi anakuwa na sababu. Kama unasema mlishaombana radhi na yakaisha, kuna kitu kimemsukuma afanye hivyo. Yawezekana kuna kitu umemkosea au amekibaini baada ya kupatana kwenu.

Tafuteni muda ili mzungumze. Tumia lugha ya kubembeleza, mueleze kwamba kama kuna sehemu umemkosea, akueleze ili umuombe radhi tena yaishe. Kama atakuwa hakutaki, hawezi kukubali kukutana na wewe na kufanya mazungumzo.

Au hata mkikutana, hatakuwa radhi kukueleza kosa lako. Ukiona hivyo, anza kupiga moyo konde na kumuweka pembeni mpaka pale yeye atakapokutafuta na kukuomba radhi.


Loading...

Toa comment