Ushindi wampa kiwewe Mzungu Majimaji

pic+kochaAKIWA na Leseni Daraja A ya ukocha kutoka Shirikisho la Soka Ulaya (Uefa), Kocha wa Majimaji, Mika Lonnstrom amepata kiwewe siku timu yake ilipopata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Kagera Sugar.

Katikati ya wiki hii kwenye uwanja wake wa nyumbani wa Majimaji mkoani Ruvuma, katika mchezo wa Ligi Kuu Bara, Majimaji iliifunga Kagera bao 1-0 na kufikisha pointi sita.

Kilichomfanya Lonnstrom apate kiwewe ni jinsi kikosi chake kilivyouanza mchezo huo vibaya huku wachezaji wake wakicheza bila malengo wakishindwa kukaba mara zote.

Lonnstrom ambaye timu yake ipo nafasi ya tano baada ya kushinda mechi mbili sawa na Yanga, Simba, Azam FC na Mtibwa Sugar, aliliambia Championi Jumamosi kuwa: “Tulikuwa tumeshafungwa kisaikolojia.

“Kwa kweli nilishangazwa na matokeo yale kwani wachezaji wangu walianza kwa kucheza vibaya na kila nilipobadili mbinu bado mambo yalikuwa magumu hadi walipotulia baadaye kabisa na kupata bao pekee la ushindi.

“Tulikuwa dhaifu kwenye kukaba, tulielemewa muda mwingi wapinzani wetu walijaribu kutuzuia kila wakati kadiri walivyoweza lakini nadhani kwa sasa tunafuraha kutokana na matokeo yale.”

Leo Jumamosi, Majimaji itacheza na Mgambo JKT kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga katika harakati zake za kutaka kufanya vizuri katika msimu huu wa ligi kuu.

JIUNGE NA MICHEZO KIGANJANI TUMA NENO SPORTS KWENDA NAMBA 15778CHAMPIONI


Loading...

Toa comment