The House of Favourite Newspapers

USHIRIKA WAMPA MAKONDA SARUJI  ZA UJENZI OFISI ZA WALIMU DAR

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, akipokea saruji kutoka kwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Ushirika Dar es Salaam, Tumaini Wilfred.  Nyuma yao ni baadhi ya wajumbe wa vyama vya ushirika.
Hali ilivyokuwa katika tukio hilo.

 

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda,  leo amepokea tani 120 za saruji ambazo ni sawa na mifuko 2,400 ya saruji kutoka kwa vyama vya ushirika 27 vya mkoa huo vilivyoguswa na kampeni ya ujenzi wa ofisi 402 za walimu Dar es Salaam.

 

Mifuko hiyo 2,400 ina uwezo wa kufyatua matofali  70,000 ambazo zitajenga ofisi 14 za kisasa kwa ajili ya walimu.

Akipokea mifuko hiyo, Makonda amesema shughuli ya ujenzi wa ofisi za walimu inaendelea vizuri  ambapo amewashukuru wadau wote wanaoendelea kuchangia kampeni hiyo inayolenga kuboresha mazingira ya kazi kwa walimu ili waweze kutoa elimu bora kwa wanafunzi na mwisho wa siku kuwe na wataalamu wa kutosha.

 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jukwaa la Ushirika Dar es salaam, Tumaini Wilfred,  amesema wameguswa na jitihada zinazofanywa na  Makonda katika kuboresha mazingira ya walimu na ndiyo maana wameona wasibaki nyuma  juu jambo hilo linalolenga kuleta ukombozi wa fikra.

 

Aidha Tumaini amesema ushirika  huo utaendelea kuunga mkono kwa kila hali  juhudi zinazifanywa na mkuu huyo.

Comments are closed.