The House of Favourite Newspapers

Usichepuke kwa udhaifu wa mkeo faragha, mfundishe!

f6a55__Lover-Couple-HD-Wallpapers-1080p-1024x5761Asalam alaikum wapenzi wasomaji wangu, naimani mu wazima mnaendelea vema na ujenzi wa taifa letu hakika mtakuwa mmejipanga vizuri kutimiza agizo la usafi la Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli .

Mimi namuunga mkono moja kwa moja kwani usafi kwa jiji letu ni muhimu sana na si kwa jiji tu hata majumbani kwetu mpaka vyumbani.

Nimeamua kukumbushia hili kabla sijaingia kwenye mada moja kwa moja kwani wanawake wengi tunatia aibu kwa uchafu na wanaume hushindwa kuvumilia hali hii na kama akipata mtu anayejua usafi ndiyo utamsahau kabisa.

Niingie kwenye mada moja kwa moja inayowagusa wanaume wetu, wanaume wengi ni wepesi wa lawama kwa wake zao na huwa wanatafuta visingizio hasa wanapokuwa wameshaamua kuhamia kwa mwanamke mwingine.

Wiki iliyopita nilipokea ujumbe kutoka kwa msomaji akisema kuwa mke wake hajiwezi faragha hivyo ameamua kuchepuka.

Niwaulize tu wasomaji wangu, nyie akina baba hivi ukichepuka ukakuta na huko hakuna kitu utahama tena? Je, utahamia kwa wanawake wangapi kisa tu kikiwa ni ujuzi, kwa nini usimfundishe na kumuelekeza mkeo unachotaka ambacho kitakufurahisha? Je, ulishawahi kufanya hivyo hata mara moja akashindwa na je, ulishawahi kumpa pesa na kumwambia atafute mtu wa kumfundisha akakataa? Kwa nini unamtesa hivyo huku wakati mwingine unaamini kabisa hana kosa kubwa alilokufanyia.

Wanaume mkumbuke hakuna aliyezaliwa anayajua mapenzi, pia wapo wanawake wanaoolewa bila kupitia kwa kungwi, sasa ni jukumu lako kumueleza mkeo au mpenzi wako afanye nini ili akufurahishe lakini si kuchepuka tu kama mnavyofanya wengi wenu na kuleta visingizio vya mke kutokuwa mbunifu.

Hivi mke akigundua umechepuka kwa sababu hajui mambo unadhani atafanyaje? Ujue wanawake wakishajua kosa hufanya juu chini na kubadilika, akishabadilika atakuonesha ujanja wake kisha atakubwaga.

Wanaume wakifanyiwa hivyo huumia sana na ndiyo maana utasikia fulani kampiga risasi mkewe yote haya ndiyo sababu kwani mwisho wa siku anasahau kuwa yeye ndiye chanzo cha yote.

Comments are closed.