Usichokijua Kuhusu Harmonize Kukabwa Mbele ya JPM!

DAR ES SALAAM: Meneja wa staa wa Bongo Fleva, Rajab Abdul ‘Harmonize’, Beauty Mmari ‘Mjerumani’ ameeleza juu ya jamaa ambaye alimkaba msanii huyo wakati akitumbuiza mbele ya Rais Dk John Pombe Magufuli ‘JPM’.

 

Tukio hilo lililoibua sintofahamu lilijiri mapema wiki hii kwenye sherehe ya uzinduzi wa Kiwanda cha Super Doll kilichopo Vingunguti jijini Dar ambapo JPM alikuwa mgeni rasmi huku Harmonize akiwa mtumbuizaji.

 

Akizungumza na Gazeti la Ijumaa, Mjerumani alisema kuwa hawamjui mtu yule na kwamba baada ya wao kutaka kujua waliambiwa kuwa ni shabiki.

 

“Kiukweli yule mtu aliyemvamia Harmonize hatumjui, lakini baadaye tuliambiwa kuwa ni shabiki tu na hakuchukuliwa hatua zozote na watu wa ulinzi na usalama.

 

“Unajua kuna mashabiki mashabiki wengine wanakuwa na mihemko yao, sasa yeye aliona akimfuata stejini ndiyo furaha yake itakuwa imetimia,” alisema meneja huyo.

Stori:NEEMA ADRIAN,Ijumaa


Loading...

Toa comment