The House of Favourite Newspapers

USICHOKIJUA MABAUNSA WA MASTAA WA KIKE

HILI halikuwepo huko nyuma! Kwamba umkute staa wa kike yuko na bausa, ilikuwa ni jambo adimu sana, lakini sasa hivi imekuwa fasheni. Mbali na mastaa wa kiume kama Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ambaye haendi sehemu bila baunsa, sasa hivi na mastaa wa kike nao wameamua kupita humohumo, kila wawapo hasa usiku, pembeni wanakuwa na wanaume maarufu kama mbavu nene, yaani walinzi.

Kwa sasa mastaa wa kike Bongo ambao wana mabodigadi ni Jacqueline Wolper, Lungi Maulanga, Irene Uwoya, Wema sepetu na wengineo. Kinachoelezwa mara nyingi ni kwamba, sababu hasa ya kuongozana na wanaume hao ni usalama wao, kwamba wao kama mastaa wana maadui hivyo endapo litatokea la kutokea au ikitokea vurugu, basi wawe na watu wa kuwasaidia.

Lakini mmoja wa mastaa hao, Lungi Maulanga anaeleza sababu ya yeye kuwa na bodigadi akisema: “Mimi mpenzi wangu ana wivu sana, yeye ndiye aliyemuajiri huyu mwanaume ili niongozane naye kila sehemu. Sasa mimi sioni shida kwa sababu sitoi pesa mimi, zaidi najiona niko salama kila sehemu.”

Mbali na sababu hizo za Lungi, zipo sababu nyingine ambazo zinatajwa kuwa ndizo zinawafanya baadhi ya mastaa kuwa na mabodigadi kama anavyoeleza mmoja wa mastaa wa kike aliyeomba jina lisiandikwe gazetini:

“Moja, ni ile kujisikia amani, kutokuwa na hofu na kujiongezea kujiamini kwa kuwa beneti na mwanaume, tena aliyejazia. Mpenzi wako anaweza kuwa mbali na wewe umealikwa kwenye shughuli f’lani usiku, sasa ukiwa na baunsa wako kwanza anachukua nafasi ya ulinzi, lakini anakufanya ujihisi kama uko na mtu wako.

“Ndiyo maana baadhi wanapenda washikwe mikono na mabaunsa wao, washikwe kiunoni, mabegani na sehemu nyingine za mwili ili tu wasijihisi wapweke.

“Lakini pia ni ‘show off’ tu! Kuna baadhi ya mastaa wanapenda wanapofika kwenye shughuli wazungumziwe, wawe gumzo, watengeneze habari kwa hiyo watabuni vitu mbalimbali vya kuwapa kiki na ndiyo maana wengine hata bila sababu watakodi wanaume wa kuongozana nao kama mabausa na kujinadi kuwa wanawalipa pesa ndefu, kumbe ni siku hiyo tu.

“Pia kuna mastaa ambao wanavaa nguo ambazo ili wawe huru lazima wawe na watu pembeni, kwa mfano unaweza kukuta staa kavaa nguo fupi sana kiasi kwamba akidondosha kitu kuokota ni mtihani au kavaa gauni refu linalohitaji kushikiliwa, wanaume hao wanafanya kazi hiyo.”

STORI:  HAMIDA HASSAN

Comments are closed.