The House of Favourite Newspapers

Usiku wa 900 Itapendeza, Dk. Shika Kuungana na Ebitoke, Nature Dar Live

Dk. Shika.

‘BILIONEA’ aliyejizolea umaarufu baada ya kuibuka mshindi katika mnada wa nyumba za mfanyabiashara, Said Lugumi, Dk. Louis Shika anatarajiwa kuungana na mkongwe wa muziki wa Hip Hop Bongo, Juma Nature na mchekeshaji, Ebitoke, Desemba 9, mwaka huu ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani wa Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem, Dar katika Usiku wa Itapendeza.

Ebitoke.

Akizungumza na Over Ze Weekend, Mratibu na Meneja wa Dar Live, Rajabu Mteta ‘KP Mjomba’ alisema kuwa, mbali na Nature na Ebitoke wakali wengine wanaotarajiwa kutikisa katika usiku huo ni kundi zima la Jahazi Modern Taarab likiongozwa na Amigo, MC Pilipili, Twanga Pepeta ikiongozwa na Ali Choki na wengine kibao.

“Kwa mara ya kwanza Dk. Shika ataongea na wananchi ndani ya Usiku wa Itapendeza, Dar Live ambapo ataeleza kila kitu kuhusu mabilioni yake ambayo yapo mbioni kuja na kutoa hamasa mbalimbali kwa wananchi kupitia maisha yake alipotoka hadi alipo,” alisema KP Mjomba.

Na Mwandishi wetu | Gazeti la Ijumaa Wikienda| Over Ze Weekend

Comments are closed.