Christian Bella, Kadjanito, Msaga Sumu wapagawisha Dar Live

9Bella akicheza na waimbaji wake.5Mashabiki waliofurika ndani ya ukumbi huo wakiserebuka.6Christian Bella akiimba wimbo wa ‘Nani Kama Mama’.7Bella akiwahamasisha mashabiki kucheza huku akiwa na taulo mkononi.8Waimbaji wa bendi ya Malaika wakiimba na kuserebuka.3Mwimbaji Msagasumu akiwapadisha mzuka mashabiki.4…Akionyesha umahiri wake wa kunengua.1Kadjanito akitoa burudani kwa mashabiki waliofurika katika ukumbi wa Dar Live jana.2… Akiimba na kunengua.10Kadja akituzwa pesa na shabiki.

KING of the Best Melodies, Christian Bella ‘Obama’,akishirikiana na bendi yake ya Malaika Music pamoja na Msaga Sumu na Kadjanito jana katika usiku wa Idd el Hajj waliwapagawisha mashabiki vilivyo ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar.

Chipukizi watisha

Katika usiku huo uliotambulika kama Usiku wa Amerudi, pazia la burudani lilifunguliwa na chipukizi ambao walionesha vipaji vya hali ya juu katika kuimba na kucheza.

Chipukizi Small J, aliwavuta mashabiki wengi kwa kuingia na staili iliyofananisha na staa wa Bongo Fleva, Belle 9 na kufanya wengi wamshangilie.

Mbali na hapo wapo chipukizi waliofunika kama vile Bad Spence, wakali wa vinanda, na chipukizi mwenye asili ya kizungu kutoka Tongwe Records.

Pazia la chipukizi lilifungwa na msanii Galaxy ambaye aliingia kwa mbwembwe na madensa wake waliofanya ukumbi wote uvutike na kushangaa shoo ambayo mashabiki wengi hawakutegemea.

Wakali Dancer watisha kwa kucheza

Kundi la kucheza la Wakali Dancer liliingia kwa mbwembwe ambapo lilianza kwa kucheza Wimbo wa Move Bit** na kufanya jukwaa lote lilipuke kwa shangwe.

Msaga Sumu akinukisha

Bingwa wa muziki wa Singeli asiye na mpinzani, Msaga Sumu aliingia na kufanya ukumbi wote ulipukwe upya kwa shangwe.

Msaga Sumu alianza kwa kuwapiga nyimbo zake zote kali kama vile Rafiki wa Kweli kisha akafuatiwa na Naipenda Simba ambao ulifanya mashabiki wengi wajiachie kwa kunyoosha mikono juu kwa muda mrefu.

Msaga Sumu aliendelea kukinukisha zaidi kwa kugonga vionjo vya Wimbo wa Huyo Mtoto kisha akamalizia wimbo wenyewe ambapo mashabiki wengi walimtaka asishuke jukwaani.

Kadjanito awasisimua mashabiki

Staa kutoka Jumba la Vipaji (THT), Kadjanito naye alikuwa mmoja waliofunika ukumbini hapo.

Kadja aliwaduwaza mashabiki wengi kwa muonekano wake na kwakuwa ilikuwa mara yake ya kwanza kuzama katika kiwanja hicho, iliwafanya mashabiki wengi wavutike na kumshangilia kwa ikumshangaa.

Staa huyo alianza kwa kuwatupia Wimbo wa Maumivu Niache ambapo ukumbi wote ulikuwa ukiimba naye.

Baada ya hapo aliangusha Wimbo wa Sina Maringo ambao wengi walikuwa wakicheza naye jukwaani na kisha akamalizia Wimbo wa Nzogo ambao umechanganyikana na lugha ya Kisukuma.

Bella amaliza kila kitu

Burudani ilihitimishwa na King of The Best Melodies, Christian Bella ‘Obama’ ambapo walianza Malaika Music kwa kutoa bonge moja la sebene kisha akaingia Bella na kuanza kuimba Wimbo wa Amerudi uliofanya mashabiki wengi wapige kelele.

Bella aliamsha shangwe zaidi pale alipowaita wadada na kinamama wote kusogea karibu kisha kunyoosha mkono na kuanza kuimba nao Wimbo wa Nani kama Mama.

Burudani iliendelea zaidi kwa Bella kwa kukamua nyimbo zake kibao kama vile Nakuhitaji, Safari Siyo Kifo kisha akawamaliza kabisa mashabiki kwa kupiga Wimbo wa Subira aliokuwa ameshirikisha na Cassim Mganga.

STORI/PICHA: ISSA MNALLY, BONIPHACE NGUMIJE, GABRIEL NG’OSHA NA ANDREW CARLOS.


Loading...

Toa comment