IKIWA ni moja ya matukio ya kusherehekea Siku ya Wapendanao, mashabiki wa burudani usiku wa kuamkia leo walikongwa nyoyo zao kwa muziki wa Jahazi Modern Taarab ndani ya Ukumbi wa Dar Live, Mbagala Zakhem jijini Dar.
Katika shughuli hiyo ya aina yake, Jahazi waliuchafua ukumbi huo kwa burudani kali huku wakikata viuno na kutikisa nyonga, jambo ambalo lilipandisha mizuka ya mashabiki na kulivamia jukwaa mara kwa mara.
Sambamba na Jahazi, pia kulikuwa na burudani ya Singeli kutoka kwa mkali wa ngoma hizo, The King Himself, Msagasumu na vijana wake.
Burudani hiyo ilirindima ukumbini hapo mpaka majogoo huku mashabiki wakila vinono na kupiga maji.
PICHA NA SUNDAY BUSHIRI | GLOBAL TV
Comments are closed.