visa

Usiku wa Valentine… Jahazi Wakinukisha Dar Live

Taarabu likonga Dar Live.

IKIWA ni moja ya matukio ya kusherehekea Siku ya Wapendanao, mashabiki wa burudani usiku wa kuamkia leo walikongwa nyoyo zao kwa muziki wa Jahazi Modern Taarab ndani ya Ukumbi wa Dar Live, Mbagala Zakhem jijini Dar.

 

Shughuli si ya kitoto.

Katika shughuli hiyo ya aina yake, Jahazi waliuchafua ukumbi huo kwa burudani kali huku wakikata viuno na kutikisa nyonga,  jambo ambalo lilipandisha mizuka ya mashabiki na kulivamia jukwaa mara kwa mara.

Sambamba na Jahazi, pia kulikuwa na burudani ya Singeli kutoka kwa mkali wa ngoma hizo, The King Himself, Msagasumu na vijana wake.

Viuno vikitaabika.

Burudani hiyo ilirindima ukumbini hapo mpaka majogoo huku mashabiki wakila vinono na kupiga maji.

Nyonga zikishughulika.

 

PICHA NA SUNDAY BUSHIRI | GLOBAL TV

 
Toa comment