The House of Favourite Newspapers

‘Usiniseme’ Kumrudisha Mjini Dullayo

0

MKALI wa kitambo kwenye gemu ya Bongo Fleva, Dullayo (D-timining) amefunguka kuwa ngoma yake mpya ya Usiniseme aliyoifanya na produzyz Salu, itamrejesha kwenye ramani ya muziki baada ya kupotea kwa muda mrefu.

D-timing aliyasema hayo wakati akifanya mahojiano kupitia kipindi cha Mid-Morning Fresh kinachorushwa kila Jumatatu hadi Ijumaa kupita spika za +255 Global Radio chini ya wakali Darboi na Babu Ally the Best.

Dullayo alisema kukaa kwake kimya kwenye gemu kulisababishwa na vitu vingi lakini kubwa ilikuwa ni kuusoma mchezo akiwa nje ya uwanja na kuongeza kuwa Bongo Fleva ya sasa ni tofauti na miaka ya 2000 hivyo inatakiwa msanii kujipanga ili aweze kufanya vizuri.

“Usiniseme naiamini sana, ni ngoma ambayo itanirudisha tena kwenye gemu, kwa sababu ni muziki mzuri ambao unaweza kusikilizwa na kila mtu kwa sababu ya ujumbe uliomo ndani.

“Nilikaa nje ya muziki kwa muda mrefu kwa sababu kuna vitu vya kibinadamu nilikuwa napitia lakini wakati huohuo nililkuwa nalisoma gemu linaendaje, unajua muziki wa sasa tofauti na zamani, lazima utulize akili kama ambavyo nimefanya kwenye Usiniseme,” alisema Dullayo.

Mbali na hivyo Dullayo aliishukuru +255 Global Radio kwa kumpa nafasi ya kutambulisha wimbo wake mpya, pia akiishukuru Global Tv Online kwa kumshika mkono baada ya kuuweka wimbo huo kwenye akaunti yake ya Youtube.

 

Dullayo ambaye aliwahi kutamba na mikwaju kama Bila Yule, Naumia Roho, Mida ya Kazi na mikwaju mingine, amewaomba mashabiki kumshika mkono na kumpokea tena kwa sababu atafanya kazi nzuri kama ambavyo ilikuwa kipindi cha nyuma.

Stori: Issa Liponda

Leave A Reply