Usipige Bwana…Tuma Meseji!-21
ILIPOISHIA GAZETI LA IJUMAA:
“Plz njoo nyumbani sasa hivi ufurahie dunia nyingine kutoka kwa Nancy na ndiyo utajua kumbe umekuwa ukikosa raha kwa muda mrefu.”
JIACHIE MWENYEWE SASA…
Bony alihisi joto la mwili likiongezeka baada tu ya kusoma meseji ya Nancy, alijiweka sawa akamjibu…
“Nakuja baby.”
Ilibidi Bony akose cha kusema kwani tangu Nancy alipojigonga kwake, amehisi kubadilika hata kimtazamo. Bony hakuwahi kufikiria hata siku moja kwamba kuna siku atakuja kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Nancy.
Moyoni alimpenda sana Nancy tangu alipomwona siku ya kwanza. Lakini alijua hawezi kumnasa hata iweje kwani alionekana ni mwanamke mwenye msimamo na kujiamini.
Sasa kuja kumsikia Nancy mwenyewe anajigonga kiasi kile, kwake ilikuwa furaha kutoka moyoni kama siyo kwenye roho!
“Baby,” Bony alimwita Neema…
“Niambie sweet…”
“Mimi nakwenda kwa Anthony mara moja lakini sikai sana.”
“Poa baby, mpe hai!” alisema Neema.
“Bi mdogo baadaye basi,” Bony alimuaga na Aisha…
“Isijekuwa unakwenda nyumbani kwa bi mdogo mwingine huko halafu unajifanya unakwenda kwa Anthony,” Aisha alitania katika ukweli uliotimilika.
Bony aliachia tabasamu laini lakini lililojaa aibu kubwa kwani ukweli ni kwamba, Bony alikuwa anakwenda nyumba ndogo nyigine ambaye ni Nancy…
“Sweetheart niko njiani nakuja,” Bony alimsukumia meseji Nancy…
“Karibu sana darling wangu…najisikia mwanamke mbele ya wanawake wengine sasa,” alijibu Nancy akiwa kweli anahisi furaha ya moyo.
***
Dakika kumi baada ya Bony kutoka, Neema alipata wazo, akamwambia Aisha…
“Aisha unajua Nancy ni mtu wangu wa karibu sana…sasa kwa yaliyotokea dhamira inaniambia niende kwake nikamwombe radhi, we unasemaje?”
Aisha kwa vile alikuwa hampendi kabisa Nancy alionesha mtazamo tofauti, akasema:
“Kwangu mimi nisingekwenda kumwomba radhi kwa sababu hatukumtaja jina…ila kama unaamini kwenda kumwomba radhi ndiyo sawa utajua mwenyewe, ila kumbuka kumfungia safari ni kumpa libichwa.”
Neema alijifikiria kwa muda lakini mwisho wa siku akasema:
“Hapana, ngoja tu niende mimi Aisha kama kwako kuna ugumu we pumzika…”
“Mimi wala siyo suala la ugumu tu, sina nafasi ya kumfuata kahaba mkubwa yule,” alifyatuka Aisha…
“He! Mara hii Nancy amekuwa kahaba Aisha?” alihamaki Neema…
“Ha! Kahaba tu, we humuoni vaavaa yake bwana.”
***
Bony alikuwa kwenye kochi kubwa sebuleni akikandwakandwa sehemu mbalimbali za mwili na Nancy…
“Hii ndiyo shikamoo yangu kwako baby, kuna mazito zaidi yanakuja,” Nancy alimwambia Bony kwa sauti iliyoashiria mahaba mazito.
Moyoni Bony akasema…
“Kama hii ndiyo shikamoo je, marahaba itakuaje?”
Bony wakati huo aliegesha gari nje nyumbani kwa Nancy akiwa hana wasiwasi. Viatu alivivua mlangoni kutokana na hali ya hewa ya mvua kuwa na matope…
“Sasa baby naomba twende chumbani,” alisema Nancy…
“Poa.”
Nancy alisimama, akamsimamisha na Bony, akasimama mbele yake akatega mgongo…
“Njoo nikubebe my dear kwenda chumbani,” alisema Nancy akiwa ameinama kidogo…
“Sweet unataweza kunibeba kweli lakini? Mimi mzito bwana,” alisema Bony akiwa anajiandaa kumrukia mgongoni. Akaruka.
Nancy alijiimarisha kinguvu kwani alimudu vyema kumbeba shemejiye huyo mpaka chumbani, akamkalisha kitandani…
“Ngoja nikafunge mlango sweetheart,” alisema Nancy akitoka.
Bony alimkuta Nancy akiwa ndani ya kipande kimoja tu cha kanga, ukijumlisha na wowowo na umbo lake nambari nane, weee..!
Wakati anatoka kwenda kuufunga mlango, Bony alimtupia macho ya mshangao…
“Looo! Loo! Looo! Acha kabisa,” Bony alijikuta akisemea moyoni…
“Ila kuna mademu wameumbwa aisee! Hawa ndiyo wale ambao katika siku sita za uumbaji wa Mungu, wao waliumbwa siku ya kwanza asubuhi…mtoto amekatika katikati halafu eti nimwache…naanzaje kwa mfano?”
Nancy aliingiza viatu vya Bony, akaviweka nyuma ya mlango, akafunga mlango, akaingia chumbani akiwa mwenye amani ya moyo kwa mambo mawili…
“Mh! Hii ndiyo dawa yake Neema, yaani anadiriki kunisengenya mimi akiwa na kahaba yule..! Halafu kama yule kahaba anajiamini ye ni mzuri, basi mimi ni mzuri zaidi yake, sasa Bony yuko kwangu.”
Nancy alipofika chumbani, alichojoa kanga akairusha kule, akaelekea kitandani, mara simu yake ikaita akaona aipokee kwanza…
“Nancy nakuja kwako bwana, niko njiani…”
Je, nini kiliendelea hapo? Usikose kusoma kwenye Gazeti la Ijumaa, Ijumaa ijayo.