The House of Favourite Newspapers

Usipige Bwana…Tuma Meseji!-4

0

ILIPOISHIA GAZETI LA IJUMAA WIKIENDA:
Mabusu hayo yalimsisimua Aisha, akajikuta amemkodolea macho Bony huku akimwambia…
“Shemeji sitaki huko.”
“Hutaki nini..?”

“Kunipa mabusu.”
“Aaah! Sasa wewe mke gani hujui kupigwa mabusu…hebu pokea na hilo,” alisema Bony na kumpiga busu jingine la nguvu zaidi.
JIACHIE MWENYEWE SASA…

“Ha! Shemeji, unaanza siyo…unaanza?” alisema Aisha kwa sauti kama ya kuhisi kuhujumiwa…
“Nimeanza nini?”
“Kunipiga mabusu?”
“Unataka kulipa kisasi au?”

“Ndiyo maana yake, si umeanza mwenyewe wakati mimi sitaki,” alisema Aisha akimfuata Bony ambaye alionesha ishara ya kukimbia.
Ilibidi Aisha amkimbize ili eti amkamate na kumpiga mabusu kama alivyofanya yeye maana ndiyo ameanza…

“Simama nakwambia shemeji,” alisema Aisha akikimbia…
“Nimesema simama shemeji…ohoo!”
Bony alikimbia hadi stoo, kabla hajaingia, Aisha alimkaribia, akamchenga na kukimbilia bafuni, Aisha akamfuata, akatoka na kukimbilia sebuleni, Aisha huyo. Ikabidi Bony akimbilie chumba cha wageni, akaingia humo, Aisha naye akazama.

Ikawa sasa Bony hana pa kukimbilia, akasimama akihema…
“Si ulianza mwenyewe shemeji?” alisema Aisha, akamshika Bony na kuanza kumpiga mabusu…
“Mmmwa…mmmwaaaaa…mmmmmmwa!” mfululizo.
“Mmmh!…mwaa!” Bony naye akajirudishia, mwishowe wakajikuta wakirudishiana. Wakazama…wakazamishana!

Walijikuta sasa wapo kwenye hatua nyigine ya denda! Ukimya ulitawala, wakasikika wakiguna tu! Miguu ilikanyaga chini mpaka wakashindwa kuhimili, wakajikuta wakiangukia kitandani puu…
“Shemeji,” Aisha aliita kwa sauti ya chini sana…
“Yes,” aliitika hivyo Bony…

“Unajua tuko kwenye hatua ya hatari sana?”
“Ni kweli, ya hatari sana shemeji.”
“Sasa tutafanyaje?” aliuliza Aisha…

“Mh! Shemeji inatakiwa umakini wa hali ya juu. Itawezekana kweli?”
“Itawezekana shemeji endapo kila mmoja ataliweka moyoni hili tukio.”
“Na unadhani inawezekana akatokea mmoja asiliweke moyoni?”
“Noo! Si rahisi, ni hatari sana kwetu.”

Wakaacha mazungumzo, wakarudia denda. Ukimya ukatawala tena, mihemko ikashika nafasi yake lakini Aisha akajitoa ili aseme…
“Shemeji…”
“Niambie.”
“Tunajiridhishaje kwamba Neema yupo ofisini saa hizi? Je, kama katoka anarudi home?”
“Si rahisi shemeji.”

“Ndiyo maana nimesema tunajiridhishaje?”
“Mpigie,” alishauri Bony.

Aisha alitoka kitandani huku akisema…
“Ngoja nikachukue simu basi.”
Bony alibaki kule chumbani. Moyo ulikataa sana kushiriki tukio lile la usaliti kwa rafiki yake na mke wake kipenzi, Neema lakini mwili wake ulikuwa radhi. Ukatokea ushindani…

“Noo…nitakuwa simtendei haki rafiki yangu Mudy. Je, ikitokea mimi nimesafiri Neema aende akaishi kwake naye amfanyie hivihivi?” alijiuliza sana Bony.
Mara, Aisha akaingia huku akiongea na simu kwa kuweka loud speaker…
“We bibie mchana tunapika nini?”

“Kuna vipande vya kuku vilibaki kwenye friji, lakini jikoni kuna viungo vyote. Ila huyo mumeo huwa hapendagi kula chakula chenye mchuzi…”
“Namjua vizuri sana mume wangu huyu…”

“…enhee! Kwa hiyo vipande vichache vya kuku kaanga, vichache unga mchuzi kwa ajili yetu. Lakini nilipanga jioni ya leo tutoke tukapate dina mahali penye utulivu,” alisema Neema…
“Oke poa…kwa hiyo kama ni chakula cha mchana tu?”
“Mchana tu Aisha,” alisema Neema…
“We unarudi muda gani sasa?”

“Mimi saa saba na nusu ndiyo natoka huku,” alisema Neema. Aisha alimtakia kazi njema na kukata simu.
Aisha aliiweka simu kwenye stuli pembeni ya kitanda, akapanda kitandani ambako Bony alikuwa amelala chali akisikiliza mazungumzo yao…

“Si umeona sasa, uhuru ni mkubwa sana,” alisema Aisha akiingiza mkono kwenye singilendi ili apate nafasi ya kukipapasa kifua cha Bony.
Walizungushana hapo, wakahamasishana, wakazama kwenye mahaba mazito huku Aisha akijiachia kwa umakini kwani muda mwingi alionekana kuweka masikio sawa kusikiliza nje…
“Shemeji, hebu sikiliza kwanza…kama mlango mkubwa unafunguliwa,” alisema Aisha.

Je, nini kiliendelea hapo? Usikose kusoma chombezo hili jipya kwenye Gazeti la Ijumaa Wikienda, Jumatatu ijayo.

Leave A Reply