The House of Favourite Newspapers

Usipige Bwana…Tuma Meseji!-5

0

ILIPOISHIA GAZETI LA IJUMAA:
Walizungushana hapo, wakahamasishana, wakazama kwenye mahaba mazito huku Aisha akijiachia kwa umakini kwani muda mwingi alionekana kuweka masikio sawa kusikiliza nje…
“Shemeji, hebu sikiliza kwanza….kama mlango mkubwa unafunguliwa,” alisema Aisha.
ENDELEA MWENYEWE…

“Unapoteza muda shemeji. hujui?” alisema Bony akiwa ameamua kulipuka tu. Liwalo na liwe!
Kazi ilianza hapo, wawili hao walizama katika usaliti mkubwa huku muda mwingi wakionyana kwamba watunze siri hiyo…

“Lakini baby itabidi tujitahidi sana kutunza siri hii,” alisema kwa kubabaisha Aisha.
“Ni kweli, yaani tunawakosea sana wenzetu…sijui tumefikaje huku?” alisema Bony.
“Si ndiyo maana nikakwambia Mudy kukaa muda wote kule ni tatizo, nilikuwa namaanisha mambo kama haya.”

“Da! Lakini leo iwe mwanzo na mwisho shemeji.”
“Kabisa…tusishikaneshikane tena sweet kwani ndiyo kumezaa yote haya,” alisema Aisha.

Mpaka mwisho wa mchezo, Aisha alimshukuru Bony kwamba amemtendea haki na akasema anaamini baada ya hapo, atatubu dhambi hiyo na kuendelea na maisha ya ushemeji kama awali.
“Shem please, leo iwe mwanzo na mwisho. Unajua tumemkosea sana Neema?” alisema Aisha akiwa anavaa.

“Ni kweli kabisa shemeji…daaa! Uso utatusuta.”
***
Saa nane, Neema alirudi nyumbani na kumkuta mumewe anaangalia tivii sebuleni huku Aisha akiwa chumbani amelala.

“Mmm…mwaa! Baby vipi? Uko poa?” Neema alimpiga mabusu mumewe na kumsalimia.
“Mmm…niko poa mke wangu. Pole kwa kazi.”
“Kazi ilikuwa njema…vipi Aisha?”

“Aisha nadhani amelala, muda mrefu sijamwona,” alisema Bony.
Neema alitoka kwenda chumbani kwa Aisha. Nyuma, mumewe akawa anamwangalia sana na kutingisha kichwa cha kujisikitikia kwa dhamira kutokana na kitendo alichokifanya.

“Da! Shetani naye, ana nguvu zake jamani!” Bony alisema moyoni…
“We mke mwenzangu,” Neema aliita huku akisukuma mlango.
Alimkuta Aisha amelala kifudifudi.
“Vipi Asha, uko poa?”

“Niko poa Neema,” Aisha alijibu huku akiangalia godoro.
“Unaumwa nini?”
“Hapana, usingizi tu Neema.”
“Lo! Pole sana…maana nashangaa unaongea huku umeinamia godoro.”
“Wala,” alisema Aisha huku akigeuka na kulala upande. Alimwangalia Neema kwa macho ya kuiba na ka aibu kwa mbali.
“Mimi ndiyo nimerudi sasa.”

“Pole na kazi Neema.”
“Asante, ngoja nibadili nguo basi.”
“Sawa Neema.”
Neema alienda chumbani lakini moyoni akahisi kuwa, Aisha hakuwa sawasawa.
“Au amemkumbuka mumewe?”

“Lakini kumkumbuka mumewe kwa siku moja tu, sidhani,” alijiambia moyoni Neema.
Baada ya kubadili nguo, alikwenda sebuleni.
“Baby, we unavyoona Aisha yuko sawasawa kweli?” aliuliza Neema akikaa jirani na mume wake.

“Kivipi baby?”
“Nimemkuta kule chumbani kama hana amani.”
“Mh! Au amechoka tu! Maana ni muda aliingia huko chumbani, mi nilijua amelala,” alisema Bony huku moyoni akisema…
“Si anaona aibu…amekusaliti mwenzako.”

Yaliisha, Neema na mume wake walikaa na kuzungumza mambo yao huku wakichombezeana na mabusu kwa mbali.
Baada na nusu saa, Aisha alitokea sebuleni.
“Nawaona wenyewe,” alitania.

“Kwa raha zangu. Nimekuachia tangu asubuhi, sasa zamu yangu. Kama ulishindwa utajiju,” alisema Neema.
Aisha akacheka kwa mbali, moyoni akasema…
“Nishindwe nina kichaa. Muulize mwenyewe tumefanya nini leo kule chumbani. Chezea mimi wewe!”

Lakini kwa sauti akasema…
“Ha! We kuwa naye tu, mimi amenichosha kabisa. Natamani hata anipe talaka yangu.”
“Talaka umepata mama, tena hakuna kurejeana, Bony naye alimtania Aisha shemejiye huku akimwangalia, walipogongana macho, Aisha aliyakimbiza haraka sana kitendo ambacho Neema alikiona, akakishangaa.

Je, nini kiliendelea hapo? Usikose kusoma chombezo hili jipya kwenye Gazeti la Ijumaa, Ijumaa ijayo.

Stori: DUSTAN SHEKIDELE, Wikienda

Leave A Reply