The House of Favourite Newspapers

USIPOKUBALI UDHAIFU HAMTOPATA FURAHA!

NI matumaini yangu kwamba mpenzi mso­maji wangu uko vizu­ri, na unaendelea salama na mishemishe zako

Siku ya leo, nitazungumzia suala ambalo husababisha mahusiano ya watu wengi kukosa mvuto, fu­raha na kuwa yenye majuto. Suala lenyewe ni la mpenzi kutokubali ud­haifu wa mwenza wake.

 

HILI NI TATIZO KUBWA

Unajua katika uchunguzi niliou­fanya nimegundua mara nyingi kati­ka suala hili watu wengi huwa hawa­gundui kama wapo kwenye tatizo.

 

Kwa mfano mdogo tu; Unakuta mpenzi wako anapenda kucheka. Ukizungumza suala lolote hata kama si la kuchekesha, yeye anach­eka au kutabasamu.

 

Hii linaweza kwa namna moja au nyingine likawa linakukera. Ukamwambia mara moja au mbili kwamba hupendi, kwa sababu ni tabia yake au udhaifu wake, anashindwa kujikontroo. Mwisho wa siku linakuwa ni suala la kuwago­mbanisha.

 

Mfano mwingine unaweza kuwa ni kwenye masuala ya mapishi. Pen­gine mwanamke unayempenda si mtu wa kupika vyakula vya kukuko­sha roho.

 

Unaumia na kujiuliza unampenzi wa namna gani asiyejua kupika. In­afika wakati badala ya kula kwake unapita sehemu fulani na kujipigilia. Migogoro ndiyo inaanzia hapo ana­pofahamu.

 

Ukweli ni kwamba mifano ni min­gi, ipo mingine ni mifano ya vitu vi­dogovidogo, kama uchafu, kuwa na mwenza asiyejali, yeye akifika ndani akivua shati anarusha popote, ak­ishika sahani anaacha popote pale na hata kwenye suala zima la tendo la ndoa. Unaweza kuwa na mpenzi mwenye udhaifu katika sehemu fulani ambayo wewe ndiyo inakufurahisha.

 

Kutokana na udhaifu wake huo, inasababisha mnafikia hatua mnakuwa hamna fura­ha na raha kwenye uhusiano wenu.

UFANYEJE LINAPOTOKEA SUALA HILI?

Jibu ni kwamba kwanza kubaliana na udhaifu wa mpenzi wako.

Baada ya kukubali taratibu mwambie ki­nachokupa furaha kupi­tia tatizo hilo badala ya kumfokea au kumweleza maneno ya kukasirisha.

Kwa mfano; “Mpenzi ninapenda sana unavyonijali, lakini hiyo haitoshi pale unapokuwa hujali vitu vyako. Si vizuri kuacha soksi mezani. Uki­vua viatu v i w e k e m o j a k w a moja kwenye henga.”

K w a l u g h a kama hii hakuna

ambaye atachukia kwa hicho uli­chomwambia. Lakini vuta picha ukimwambia hivi;

“Hivi wewe mwanaume mbona huko hivyo, yaani uchafu umekuz­idi kha! Mpaka soksi unaacha po­pote kiukweli umenishinda tabia.”

Kwa maneno haya hata kama kile unachoeleza ni sahihi lakini kwa uwasilishaji huu utakuwa unatengeneza jipu. Kwanza huyo mwanaume akilini mwake atafiki­ri humuheshimu, unaongea sana au hujafunzwa.

Wapo wengine ukimwambia hivyo atakurudia kwa maneno; “Kwani nikiweka kitu vibaya hu­wezi kutoa, kazi yako ni nini sasa hapa?”

Wewe utajibu; “Kwa hiyo kazi yangu ni kuokota soksi zako?”

Kwa hiyo mtajikuta mnajibisha­na maneno mwisho wa siku kila mmoja anakasirika na kunakuwa hakuna furaha tena. Kwa hiyo kukabiliana na changamoto ya udhaifu wa mpenzi wako, kwanza halafu tumia lugha nzuri kuitatua, kwa kumfundisha au kumuele­keza.

Comments are closed.