The House of Favourite Newspapers

Usitegemee kupata kila kitu darasani

0

Suala la mwanafunzi kujifunza ni endelevu, halina kikomo na kamwe haliishii darasani kama wanafunzi wengi wanavyofikiria.

Mwanafunzi mwenye malengo ya kufaulu na kufika mbali kielimu hutakiwa kuweka juhudi zaidi katafuta ‘material’ baada ya muda wa darasani. Ikiwemo mitihani iliyopita (past papers), vitabu vya majaribio na majibu (parfects) na hata kujibrashi kwenye topiki ambazo darasani hakuzisoma ipasavyo.

Wanafunzi wanapaswa kukumbuka walimu wengi darasani hasa hukimbizana na muda. Wanachohitaji wao ni kufikia muda fulani kuhakikisha wamefundisha topiki kadhaa, basi!
Sasa ni muhimu kufahamu juu ya hilo, na uzuri wa mitihani ya nyuma hutoa mwelekeo wa nini hasa mwanafunzi anatakiwa kukifanyia kazi zaidi. Kwa hiyo kama nihivyo ukiona darasani kile ambacho unatakiwa kukifanyia kazi hujakipata ipasavyo changamka kwa kujiongeza zaidi nje ya darasa.

Kwa wanafunzi wanaosoma wakiishi nyumbani wanaweza pia kushirikiana na wanafunzi wenzao wa shule zingine kubadilishana material.

Mwanafunzi atakayezingatia haya atajiwekea nafasi nzuri ya kufanya vyema kwenye masomo yake.

Leave A Reply