Yajue Madhara ya Kutumia Smartphone Gizani
PALE taa zinapokuwa zimezimwa usiku, usiitumie simu yako ya mkononi (smart phone). Huo ni ushauri uliotolewa na taasisi moja ya uchunguzi.
Kutumia simu kabla ya kulala huku taa zinapokuwa zimezimwa, kunaweza kusababisha matatizo.
Hivi sasa idadi ya wagonjwa wenye kuanzia umri wa miaka 30 hadi 40 wanatafuta matibabu kutokana na matumizi ya simu za mkononi (wakati wa giza
Dakrari mmoja wa hospitali ya macho nchini Singapore anasema: “Mionzi ya moja kwa moja kwa zaidi ya dakika 30 kwenda kwenye macho inaweza kusababisha mpangilio na mbadiliko wa seli za macho na hivyo kusababisha saratani ya macho na kushindwa kuona kabisa.
Kupata saratani ya macho inamaanisha kupoteza kuona kwa sababu utaalamu wa afya kwa sasa hautibu saratani hivyo ni bora kuacha kutumia simu za mikononi gizani ili kujikinga.
Simu za mikononi zenye mwanga mweupe sana karibu na macho gizani, hubadili mfumo wa seli za macho na kusababisha saratani ya macho.
Profesa huyo amesema dalili za mbadiliko wa seli za macho mara nyingi wanazigundua watu wenye umri mkubwa (wazee), ila kwa hivi sasa zinagunduliwa hata na kwa vijana wadogo, hasa kwa wenye umri wa kuanzia miaka 30 hadi 40 ambao wanaongezeka kwa asilimia 3% ambapo wote hawa ni watumiaji wakubwa wa simu hizo.
Hata hivyo, kutumia simu gizani si sababu ya tatizo la kusababisha saratani ya macho tu, bali kunaweza kusababisha matatizo mengine ya macho kama vile mtoto wa jicho na mwisho kusababisha kuona.
Dalili za mwanzo, kama vile vipele vidogo-vidogo, huwa zinatibiwa kwa mionzi, sindano na madawa.
Madaktari bingwa wa macho wanahimiza kwamba ni muhimu kutotumia simu gizani ili kukwepa matatizo hayo.
Comments are closed.